Manchester City imeendelea kuwa mshindani mkuu wa Arsenal kileleni, baada ya kuifunga Cardiff City mabao 4-2 jana jioni Uwanja wa Etihad.
Edin Dzeko alifunga bao la kwanza dakika ya 14, pasi David Silva, Noone akawasawazishia wageni dakika ya 29 pasi ya Gunnarsson kabla ya Jesus Navas kuwafungia wenyeji la pili dakika ya 33.
Kipindi cha pili, City waliingia na moto na kupata bao la tatu dakika ya 77, mfungaji Mwanasoka Bora wa Afrika, Yaya Toure, pasi ya Sergio Aguero. Aguero aliifunga bao la nne City dakika ya 79, pasi ya Yaya kabla ya Campbell kuifungia Cardiff la pili dakika za majeruhi, pasi ya Eikrem.
Ushindi huo unaifanya City ifikishe pointi 50 baada ya kucheza 22, tofauti ya pointi moja na vinara Arsenal.
kocha wa Man City Manuel Pellegrini akitweta na Sergio Aguero
kocha wa Cardiff city
Sergio Aguero akiifungia Man city goli la nne dakika ya 79
Mechi nyingine za ligi kiuu ya England zilizochezwa jana jioni,
Sunderland ilitoka sare ya 2-2 na Southampton,
Crystal Palace imeifunga 1-0 Stoke City,
Norwich City imeifunga 1-0 Hull City na
West Ham United imelala 2-1 dhidi ya Newcastle United.
Post a Comment