Jifunze leo
Maisha ya kisasa ambayo tumeiga kutoka nchi za Magharibi kwa mfano, Marekani yamechangia sana kuharibu utamaduni wetu na malezi kwa watoto.
Tukinzungumzia malezi, wazazi au kinadada wengi wanaonekana kuzidiwa nguvu na utamaduni wa nchi za Magharibi.
Wapo baadhi ya kinadada wathubutu kusema kwamba akijifungua mtoto, hatanyonyesha, wengine wanasema watanyonyesha miezi miwili tu na kumuachisha ziwa mtoto.
Sababu kubwa, wanasema wakinyonyesha matiti yao yatashuka na kupoteza shepu. ‘Kaka urembo mali,’ anasema Asha Sisiko Nderikiayo.
Lakini madaktari wanaonya kwamba mama ambaye hanyonyeshi, mtoto au watoto wanakuwa katika hatari ya kuambukizwa magonjwa mbali mbali.
Daktari wa watoto katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dk Massawe anasema maziwa ya mama ni kinga kwa mtoto.
Dk Massawe anasema mtoto wa umri sifuri mpaka miezi sita, anatakiwa kunyonya maziwa ya mama tu bila kumpa aina yoyote ya chakula.
Baada ya miezi sita mtoto anapaswa kula vyakula vya aina nyingine kwa mfano, uji wa dona, uji wa lishe, ndizi, nyama ya kusaga, mboga za majani na samaki huku mama akiendelea kunyonyesha.
Matunda ambayo watoto wanatakiwa kula ni papai, parachichi, tikiti maji, ndizi mbivu, na embe.
Wazazi wanapaswa kuonana na madaktari wa watoto na kupata ushauri zaidi jinsi ya kutengeneza vyakula hivyo.
Endapo wazazi watazingatia ushauri wa madaktari wa watoto, watafanikiwa kujenga afya bora kwa watoto wao.

Post a Comment