SENTAHAFU wa Brazil anayekipiga Bayern Munich Dante amekiri kuwa Manchester United wanajaribu kumnunua.
Beki huyo mwenye umri wa miaka 30 alikuwa akizungumza na Fox Sports huko nyumbani Brazil ambapo mtangazaji aliyekuwa akimhoji akatangaza kuwa nyota huyo anakaribia kumalizana na Manchester United.
Alipoulizwa kama tayari ameshasaini kwa vijana wa David Moyes, Dante akasema “bado” lakini akakiri kuwa kuna ushawishi kutoka kwa mabingwa hao wa England.
“Nashukuru kwa Manchester United kuvutiwa na mimi, kila kitu kitakuwa kimetatuliwa mwisho wa mwezi.”
Beki huyo wa zamani wa Borussia Moenchengladbach amecheza mechi 15 kati ya 16 za Bayern msimu huu.
Post a Comment