MZEE AUMBUKA BAADA YA KUNASWA NA DENTI GESTI LAIVU!

Tabia ya wazee ya kupenda dogodogo imemtokea puani mzee aliyetajwa kwa jina moja la mzee Omari,
            Babu akifunika uso wake baada ya kunaswa na denti gesti.

Mzee huyo alinaswa laivu akiwa gesti na denti wa shule moja ya sekondari jijini Dar (jina la denti na shule vinahifadhiwa kimaadili).
Tukio hilo la aibu lilijiri juzikati kwenye gesti moja iliyopo maeneo ya Kawe, Dar na kusababisha timbwili zito.
Hivi karibuni, kikosi maalum cha Oparesheni Fichua Maovu, kilipokea lalamiko kutoka kwa mzazi wa denti huyo ambaye alieleza juu ya mabadiliko ya mwanaye kitabia na kushuka kitaaluma kutokana na kusumbuliwa na ‘mbaba’ huyo.
Mzazi huyo aliiambia OFM kuwa amekuwa akifuma mawasiliano ya kwenye simu ya mkononi ya mwanaye na mwanaume huyo ambaye alikuwa hamfahamu.

        Babu akijiandaa kuvaa nguo yake ya ndani baada ya kunaswa gesti.
 

Mama huyo alisema kuwa kutokana na maendeleo ya mwanaye kuzidi kudorora shuleni, aliamua kumfuatilia kwa karibu kwa kuwa hakutaka apotee siku ya tukio, alimsikia mwanaye huyo akiwekeana miadi kwenye simu na mwanaume huyo ndipo akaamua kumuwekea mtego.

Alisema wakati mwanaye huyo akilonga kwenye simu, yeye alibana sehemu na kuyasikia yote ambayo alikuwa akiyaongea na kwamba walipanga kukutana baa.

“Nilichokifanya nilimpigia simu mjomba wake na kumweleza kila kitu, nikamwelekeza namna ya kumfuatilia. Alichukua bodaboda na kuanza kumfuatilia. Mimi na timu yangu tulifuata nyuma,” alisema mama huyo kwa uchungu.

                           Babu akiwa mikononi mwa wanausalama.

Alisema mzee huyo alikubaliana na mwanaye wakutane kwenye baa hiyo ambapo ndani yake kuna nyumba ya kulala wageni a.k.a gesti.
Baada ya mpango wa mtego kukamilika ndipo mama huyo akawaita OFM ambao huwa hawalazi damu hivyo walifika mara moja.
Kabla ya kuchukua hatua yoyote, walishauriana kutoa taarifa kituo cha polisi, jambo ambalo lilifanyika na kupatiwa msaada wa kiusalama.
Walipofika kwenye baa hiyo mama mtu alipigwa na butwaa kumuona mtu aliyekuwa akiwasiliana na mwanaye ni mzee sawa na babu yake.
“Yaani jamani kweli dunia imekwisha, mwanangu ni sawa na mjukuu wa huyu mzee, ama kweli tamaa mbaya sana,” alisema mama huyo kwa uchungu.

Huku wakifuatiliwa kwa karibu, mzee huyo na denti walipiga madikodiko na vinywaji ndipo wakatimba kwenye gesti hiyo.
Kilichofanyika ni kwamba polisi na mama wa denti walizama gesti hiyo na kuomba kumsaka mwanafunzi huyo, jambo ambalo halikupingwa.

Baada ya kuzama ndani ndipo mtego ukafyatuka ambapo mzee Omari alibambwa katika moja ya vyumba vya gesti hiyo huku akiwa amejifunga taulo tu.
Mzee huyo alipatwa na taharuki kubwa asijue la kufanya kufuatia timbwili zito alilozua mama wa denti huyo.
“Kha! Kazi kuharibu watoto wa wenzenu, hivi angekuwa wa kwako ukakuta akifanyiwa hivi ungejisikiaje? Nasomesha kwa gharama kubwa wewe unataka kuniharibia. Hivi hujui mtoto anauma?” alihoji mama huyo kwa hasira huku akimtandika mwanaye vibao.

Mara baada ya mzee huyo kunaswa, aliomba chondechonde kukaa na familia ya mwanafunzi huyo ili kuyamaliza yasifike mbali.
Hata hivyo, baada ya maombi ya muda mrefu walikubaliana kuandikishiana ambapo mzee huyo alitakiwa kulipa faini.
“Sisi hatuna maneno mengi, hatutaki kesi ila atulipe fidia ya kumsababishia mtoto wetu asiwe na mahudhurio mazuri shuleni kutokana na ulaghai wake,” alisema mzazi huyo.


Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top