YANGA YAILAZA MBEYA CITY 1-0, NA AZAM YAFANYA VIBAYA CHAMAZI, 4-0

YANGA SC imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Pamoja na ushindi huo, Yanga inabaki nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu, baada ya Azam FC leo hii kuifunga Kagera Sugar mabao 4-0 Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam. Azam sasa ina pointi 36 na Yanga 35 baada ya kila timu kucheza mechi 16.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Abdallah Kambuzi wa Shinyanga aliyesaidiwa na Ferdinand Chacha wa Kagera na Mohamed Mkono wa Tanga, hadi mapumziko Yanga walikuwa mbele kwa bao 1-0.

Raha ya mechi bao; Wachezaji wa Yanga wakimpongeza Mrisho Ngassa wa pili kulia baada ya kufunga bao peke leo Uwanja wa Taifa

Mrisho Ngassa akimtoka beki wa Mbeya City leo

Bao hilo lilifungwa na Mrisho Khalfan Ngassa dakika ya 16, baada ya kuuwahi mpira uliorudishwa na mabeki wa Mbeya City kufuatia krosi ya David Luhende.
Pamoja na kufungwa bao hilo mapema, lakini Mbeya City walicheza vizuri na leo sifa zimuendelee kipa wa Yanga Deogratius Munishi ‘Dida’ kwa kuokoa michomo kadhaa ya hatari.
Dakika mbili tu baada ya kuanza kwa kipindi cha pili, Mbeya City walipata pigo baada ya kiungo wao tegemeo, Steven Mazanda kuonyeshwa kadi ya pili ya njano na kuwa nyekundu kwa kumtolea lugha chafu refa wakati wachezaji wa Yanga wakijipanga kupiga mpira wa adhabu.  
Pamoja na kumpoteza Mazanda, bado Mbeya City waliendelea kuonyesha upinzani kwa Yanga ambao leo walikuwa wanadekezwa na refa.


Kikosi cha Yanga SC leo kilikuwa; Deogratius Munishi ‘Dida’, Mbuyu Twite/Juma Abdul dk63, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Frank Domayo, Simon Msuva, Haruna Niyonzima, Didier Kavumbangu/Hamisi Kiiza dk70, Mrisho Ngassa na David Luhende.

Mbeya City; David Burahn, John Kabanda, Hassan Mwasapili, Deogratius Julius, Yussuf Abdallah, Anthony Matogolo, Mwagane Yeya/Saad Kipanga dk75, Steven Mazanda, Paul Nonga/Richard Peter dk63, Peter Mapunda na Deus Kaseke/Joseph Willson dk70.

Uwanja wa Azam Complex, mabao ya Azam yalifungwa na Brian Umony mawili dakika za 13 na 48, Kevin Friday dakika ya 51 na Jabir Aziz dakika ya 83.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top