Baada ya Westgate, kumetokea tukio jingine Nairobi.........Soma zaidi hapa

Baada ya tukio la Westgate ambalo liligharimu maisha ya watu wengi jijini Nairobi, kumeibuka tishio jingine la aina hiyo kwenye eneo la biashara la Nakumatt Junction Barabara ya Ngong ambapo yamekutwa masanduku manne ya kubebea risasi kwenye eneo la kuegesha magari kwenye vyumba vya chini (Basement).

Masanduku hayo yalipatikana ndani ya toroli la kubebea mzigo kutoka kwenye duka la jumla la Nakumatt ambapo walioshuhudia wamesema sanduku hizo zilikuwa zimeandikwa ‘explosion’ na walipoitwa wataalam wa mabomu  waligundua kuwa sanduku hayo yalikuwa yamebeba risasi za bunduki aina ya ceska ama Mp5 machine gun
 milimita 9.

Masanduku hayo yaligundulika wakati wafanyakazi wakirudisha matoroli hayo ndani baada ya wateja kuyatumia na kuyaacha eneo la parking.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top