YANGA SC chupuchupu kupata ajali mbaya asubuhi ya leo, Baada ya mechi yake ya jana....Soma zaidi hapa

Kocha Mkuu wa Yanga SC, Mholanzi Hans van der Pluijm akiruka dirishani kutoka kwenye basi la timu hiyo baada ya kunusurika kupinduka asubuhi ya leo eneo la Mikese, Morogoro wakati wakijaribu kukwepa basi la abiria. Yanga SC ilikuwa inatokea Morogoro ambako jana ilicheza mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya wenyeji, Mtibwa Sugar na kutoka sare ya bila kufungana.
Basi la Yanga likiwa limeinama upande mmoja baada ya kukwepa basi la abiria. Hakuna aliyeumia na timu imeendelea na safari ya kurejea Dar es Salaam baada ya mkasa huo kutokea.
Kocha Yanga Pluijm kulia akiozungumza kwa simu,  na Juma Pondamali akiwa pembeni yake.
Wachezaji wakitokea madirishani  baada ya kunusurika ajali mbaya asubuhi ya leo. 
 Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo Mikese.




TUNAOMBA MAONI YAKO HAPA CHINI KUHUSU TAARIFA HII!!! 

1 comments:

daaaaah wape pole mnooo!

Reply

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top