HOT NEWS...Ajali tena-Basi la Super feo na Upendo yagongana

Basi la kampuni ya Super Feo likiwa limegongwa kwa nyuma na basi la Upendo. Mabasi yote yanafanya safari kutoka Dodoma kwenda Iringa (upendo) na Super Feo (Songea) . Ajali hii imetokea asubuhi ya leo ikihusisha mabasi mawili ya kampuni ya SUPER FEO likitokea Dodoma kuelekea Songea na basi la UPENDO TRAVELLERS kutokea Dodoma kuelekea jijini Mbeya.
Taarifa za kutoka eneo la tukio zinasema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni punda aliyekatisha barabarani na  mwendo kasi wa basi la upendo bila umakini wa dereva wa basi hilo. Walisema abiria waliokuwa katika basi la upendo kuwa walikuwa wakilifuata basi la Super feo kwa kasi bila kuacha nafasi ya usalama kati ya basi moja na lingine nyuma au mbele hali iliyopelekea ajali hiyo kutokea pale dereva wa basi la Super feo aliposimama ghafla kuepuka kugonga punda aliyekuwa akikatisha barabarani.



Taarifa zinaendelea kudai kuwa dereva wa basi la upendo amevunjika miguu na wengine wamejeruhiwa vibaya!

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top