Kajala Masanja achaguliwa kuwa balozi wa wanawake Tanzania......

Staa maarufu wa filamu hapa Bongo, Kajala Masanja hivi karibuni alipata shavu la nguvu baada ya kuibuka kuwa balozi wa wanawake Tanzania nzima kupitia taasisi ya Women Connect iliyopo jijini Dar.

 Akizungumza na mkurugenzi wa taasisi hiyo, Hafsa Semdaiya alisema wameamua kumchagua Kajala kwa kuamini ni kioo cha jamii na ni staa wa kwanza kuonesha moyo wa kuitikia wito kwani alianza kwa kutoa misaada kwenye kituo cha watu walioathirika na madawa ya kulevya.

“Kwa kweli kigezo kikubwa tulichokiona kwa Kajala ni moyo wake wa kujitoa na pia tumemuona ni kioo cha jamii na kama mwanamke anayejali, amekuwa mstari wa mbele kwenye kutoa misaada mbalimbali kwa watu wenye uhitaji,” alisema Semdaiya.

Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa, taasisi hiyo inajihusisha na vitu vingi ila Kajala atahusika zaidi na kuchangisha fedha ndani na nje ya nchi kwa ajili ya kuwasaidia wanawake wenye vimbe mbalimbali.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top