Mechi hiyo iliyopata mshindi katika muda wa ziada, ilionekana kama Atletico wangeshinda mpaka Sergio Ramos aliposawazisha katika dakika za majeruhi.
Kabla ya hapo Diego Godin aliipatia Atletico goli la kuongoza dakika ya 36.
Gareth Bale akafunga goli maridadi kwa kichwa katika muda wa nyongeza kabla ya Marcelo kuongeza la tatu na Christiano Ronaldo kumalizia la nne kwa mkwaju wa penati baada ya kuangushwa ndani ya 18.



Post a Comment