Kesi ya mwanariadha wa Afrika Kusini, Oscar Pistorius itaendelea Oktoba 21, 2014 mawakili wake wakitaka apewe adhabu ndogo.
Mahakama inayosikiliza kesi dhidi ya mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini, Oscar Pistorius imeambiwa kuwa mwanariadha huyo amefilisika.
Pistorius alipatikana na hatia ya mauji ya mpenzi wake Reeva Steenkamp bila ya kukusudia mwaka jana.
Jaji Thokozile Masipa anatarajiwa kutoa hukumu dhidi ya Pistorius Jumanne. Anakabiliwa na kifungo cha miaka 15 lakini jaji anaweza kuamua kumpa kifungo cha nje au hata kumtoza faini. Upande wa mashitaka unataka Pistorius apewe adhabu kubwa kuambatana na kosa lake.
Pistorius aliangua kilio wakili wake alipoambia mahakama kuwa amefilisika Pistorius aliangua kilio wakili wake aliposema kuwa pesa zake zimekwisha baada ya kesi yake kufanya kwa miezi saba. "sio tu kwamba hana pesa bali anahisi hana tena matumaini,'' alisema wakili wa Pistorius.
Mwanariadha wa Afrika Kusini, Oscar Pistorius akiwa mahakamani siku ya leo. 



Post a Comment