Uvum kuhusu wolper kumpiga mizinga bwana wa Wastara.... Ukweli huu hapa



Staa wa Bongo Movies, Jacqueline Wolper amedaiwa kuwa na tabia ya kumpiga mizinga (kuomba fedha) mume mtarajiwa wa mwigizaji Wastara Juma, Mark Edi.

Kwa mujibu wa gazeti la Risasi, chanzo chao makini makini kilicho karibu na Mark ambaye ni mfanyabiashara mwenye maduka ya nguo jijini Dar, kilidokeza  kuwa, kabla ya kuanzisha uhusiano na Wastara, Mark alikuwa na uhusiano na Wolper lakini alimshindwa kutokana na tabia hiyo ya kupiga mizinga.

“Yaani Wolper ni balaa, anampiga sana mizingamizinga jamaa, mara anataka elfu 25, mara 30 yaani ni balaa tupu hadi ikafika steji Mark akaamua kumpiga chini na kutulia na Wastara,” kilisema chanzo hicho.


Baada ya kugaiwa ‘ubuyu’ huo sambamba na ushahidi wa SMS zilizoonesha Wolper akimuomba Mark fedha, mwanahabari wa Risasi alimtafuta Mark ili kuweza kujua kama madai hayo yana ukweli ambapo alipopatikana alikiri na kudai amemchoka mwigizaji huyo.

“Daah! Umezipataje hizo habari? Ni kweli Wolper alikuwa mtu wangu lakini kwa sasa sina habari naye, ni mtu muongomuongo, mizinga kila wakati hadi nikaona bora niachane naye nitulie na Wastara,” alisema Mark ambaye kwa sasa wanapika na kupakua na Wastara.

Wolper hakupatikana kuzungumzia swala hili.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top