BREAKING NEWZZ: TANZIA...Mbunge wa Ukonga, Eugene Mwaiposa afariki dunia...



MBUNGE wa Jimbo la Ukonga, Eugene Mwaiposa (CCM) aliyepo pichani, amefariki dunia akiwa nyumbani kwake mkoani Dodoma leo baada ya kusumbuliwa na shinikizo la damu kwa muda mrefu.

Taarifa iliyotolewa na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kwamba marehemu alikuwa na tatizo la shinikizo la damu kwa muda mrefu na amefariki akiwa nyumbani kwake Dodoma.

Ameongeza kuwa nyumbani kwa marehemu ni eneo la Chaduru jirani na jengo jipya la Hoteli ya Shabiby barabara ya Dar es Salaam.
Mwili wa marehemu umepelekwa hospitali ya Mkoa wa Dodoma kwa uchunguzi zaidi.

Shughuli ya kuaga mwili itafanyika kesho. Naibu Spika ametumia kanuni ya 152 kuahirisha bunge hadi keshokutwa Alhamisi kutokana na msiba huo.


Taarifa zaidi.*******************************************
Kwa mujibu wa Naibu Spika wa Bunge Mh. Job Ndugai ambaye amelitangazia bunge leo majira ya saa 7 mchana, marehemu Mwaiposa alikuwa akisumbuliwa na tatizo la shinikizo la damu kwa muda mrefu.

Ndugai amesema kuwa kwa sasa msiba upo nyumbani kwake eneo la Chadulu Dodoma ambapo pia familia yake inasubiria hapo kwa ajili ya kuaga mwili wake shughuli ambayo itafanyika kesho (Jumatano).
Bunge limeahirishwa hadi keshokutwa saa 3 Asubuhi.

Marehemu Mwaiposa alizaliwa Novemba 23, wilayani Hai mkoani Kilimanjaro mwaka 1960 na amefariki leo akiwa na umri wa miaka 44.

Alipata elimu yake ya msingi katika shule ya msingi Nkweseto mwaka 1967 hadi 1974 na kujiunga na shule ya sekondari Masama mwaka 1976 hadi 1980 ambapo baadaye alipata elimu ya juu ya sekondari katika shule ya biashara ya Shinyanga (Shycom) mwaka 1981 hadi 1983.

Amefariki akiwa na shahada mbili za uzamili, moja ikiwa ni ya mahusiano ya kimataifa kiuchumi na (Masters in International Enomic Relations) na nyingine akiipata katika chuo kikuu cha Strathclyde, kilichoko Glasgow nchini Scotland.

Enzi za uhai wake amewahi kufanya kazi taasisi mbalimbali ikiwa ni pamoja na benki ya CRDB, shule ya msingi Tumaini, Kipunguni SACCOS.

Amekitumikia Chama Cha Mapinduzi kwa nyazifa mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwa mjumbe wa Umoja wa wanawake wa CCM UWT na mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM kupitia UWT kati ya mwaka 2008 na 2013.

Mungu ametoa Mungu ametwaa jina lake lihimidiwe. R.I.P

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top