Burundi!! Zoezi la upigaji kura laanza licha ya wapinzani kuweka vitisho mbalimbali...



Baada ya ghasia na maandamano ya miezi kadhaa, hatimaye raia nchini Burundi sasa wamefika katika vituo vya kupiga kura ili kumchagua rais wao.

Kiongozi wa sasa wa nchi hiyo anawania muhula wa 3 kama rais licha ya madai kuwa anakwenda kinyume na katiba ya nchi.
Viongozi wanne wa upande wa upinzani wameapa kususia uchaguzi huo.

Rais Pierre Nkurunziza, akiwaamevalia jezi ya michezo alipanga foleni katika kituo kilichokaribu na mji wa Ngozi alikozaliwa na kupiga kura.
Waangalizi wachache mno wanashiriki uchaguzi huu baada ya serikali ya Burundi kuwanyima vibali waangalizi wa Umoja wa Afrika katika muda wa lala salama.

Hata hivyo, waangalizi kutoka umoja wa Afrika Mashariki wapo huko kwa mwaliko wa rais Nkurunziza.
Karatasi za kura zinaonesha kuwa kulikuwa na wagombea nane wa kiti cha urais lakini wanne kati yao wameshathibitisha kuwa hawatashiriki uchaguzi huo wakipinga hatua ya rais Nkurunziza kuwania muhula wa tatu. Uchaguzi huu unafanyika licha ya taharuki kuhusiana na mgogoro wa kisiasa

Wagombea hao ni Agathon Rwasa, Jean Minani, Domitien Ndayizeye na Sylvestre Ntibantunganya.

Jina la rais Nkurunziza na ishara ya chama chake imechapishwa miongoni mwa wagombea wa urais.

Saa chache tu kabla ya kufunguliwa shughuli ya upigaji kura, milipuko ya gruneti iliripotiwa jijini Bujumbura na kufuatiwa na milio ya risasi.
Rais Nkurunziza ameonekana akipiga kura karibu na mji wa Ngozi

Katika maeneo mengine risasi zilisikika kwa wingi zaidi mjini humo.

Japo haikuwa wazi ni nani hasa anayefyatua risasi hizo.
Viongozi wa upinzani wamesusia kushiriki uchaguzi huo kwa dai rais anakuka sheria kwa kuwania muhula wa tatu

Kwa mujibu wa mshauri wa kisaisa wa rais, haya ni mashambulio yanayofanywa na ‘magaidi’ wanaonuia kuvuruga shughuli ya uchaguzi.

Hofu ya kuwa uchaguzi huu huenda ukalitumbukiza taifa hilo katika mzozo mbaya zaidi wa kisiasa imeifanya jamii ya kimataifa kuitisha kuahirishwa kwa uchaguzi na kupendekeza mashauriano ya aman


Wito kama huu uliambulia patupu, mwishoni mwa wiki mashauriano ya amani yalivunjika na uchaguzi ndio huu unafanyika huku wito wa kuahirishwa kwake ukipuuziliwa mbali.

Takriban watu 70 wamefariki katika maandamano ya awali kupinga uchaguzi huu huku wengine zaidi ya elfu 160 wakiikimbia nchi kwa hofu ya kuzuka mapigano.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top