Breaking News: Waziri Celina Kombani afariki dunia nchini India

Taarifa zilizotufikia muda huu kwenye chumba chetu cha habari ni kwamba Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mh.Celina Kombani amefariki dunia nchini India alikokuwa akipatiwa matibabu

Taarifa hizo zimesema Waziri Kombani ambaye pia alikuwa mgombea ubunge jimbo la Ulanga Mashariki kupitia chama cha Mapinduzi, mwili wake utawasili nchini Jumamosi ya Septemba 26 mwaka huu

Marehemu Kombani alikuwa akiugua maleria kali,

Taarifa zaidi za kifo cha Mh. Celina Kombani
Dakika chache zilizopita baada ya kusambaa taarifa za kifo cha waziri Celina Kombani, naibu Spika Job Ndugai amezungumzia namna walivyopokea msiba huo

Ikumbukwe kifo cha Waziri Kombani kimetokea ghafla huko nchini India alikokua akipatiwa matibabu

Paparaziwetu inatoa pole kwa familia ya marehemu na taifa kwa ujumla kwa msiba huu uliowapata.


Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top