Mitambo ya kuzalisha Umeme wa gesi yawashwa,Tatizo la Umeme kukatika kuisha Leo.

Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) limesema kazi ya kuunganisha mabomba ya gesi kutoka Kinyelezi I kwenda katika mitambo ya Ubungo I na II, jijini Dar es Salaam imekamilika.

Aidha, kazi ya kuwasha mashine 10 za mtambo wa Ubungo I imekamilika na  inategemewa tatizo la kukatika umeme litafikia tamati kuanzia leo.

Akizungumza na mtandao huu jijini Dar es Salaam jana, Ofisa Uhusiano wa Tanesco, Adrian Severin, alisema kazi ya kuwasha mitambo hiyo inahitaji umakini mkubwa  kutokana na mfumo unaotumika kuwa mpya.

Alisema kazi ya kuunganisha mabomba ya gesi imekamilika na tatizo lililokuwapo la kukatika umeme lilitokana na matengenezo ya mfumo mpya yaliyokuwa yakiendelea kwa ajili ya kuwashwa kwa mitambo hiyo mipya.
Aliwataka wananchi wawe na subira wakati kazi hiyo ikiendelea na hadi kufikia leo itakuwa imekamilika na umeme utapatikana kwa uhakika baada ya kuanza kuzalishwa kwa kutumia gesi kutoka Mtwara.

 “Kuanzia leo (jana) umeme umeanza kurudi kupatikana kwa uhakika katika mikoa mbalimbali pamoja na jiji la Dar es Salaam kutokana na mafundi kufanikiwa kwa kiasi kikubwa kuwasha genereta 10 za Ubungo I, hivyo mpaka kesho (leo) uzalishaji umeme utakuwa umeongezeka,” alisema na kuongeza:

“Watanzania wategemee umeme wa uhakika baada ya kuanza kuzalisha umeme wa gesi ya Mtwara kwani  kazi ya kuunganisha bomba la kusafirisha nishati hiyo imekamilika hivyo inatuhakikishia nchi kuwa na umeme wa uhakika hata kama mabwawa ya maji yanayotumiwa kuzalisha umeme yatakuwa yamekauka.”

Severin alisema gesi ya kutoka Mtwara inategemewa kuendesha mtambo wa Ubungo II wenye uwezo wa kuzalisha MW 105, mitambo ya Symbion MW 112 na Kinyerezi I, MW 150).

Alisema mtambo wa Ubungo I utaendelea kuzalisha umeme kwa kutumia gesi ya Songosongo na kwamba Ubungo II ndiyo utumia gesi ya Mtwara kwa kuwa inatosha kuendesha mitambo hiyo.

Severine alisema uzalishaji wa umeme kwa kutumia gesi utaisaidia serikali kuokoa takribani dola za Marekani bilioni moja kwa mwaka, ambazo zilikuwa zinatumiwa kununua mafuta mazito ya kuzalisha

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top