Breaking news: Waziri Dr. Abdallah Kigoda afariki dunia

Habari zilizotufikia mda-huu ni kwamba Waziri wa viwanda na Biashara Dr. Abdallah Kigoda amefariki dunia leo saa 10 jioni huko India

Waziri huyo amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Apollo nchini India

Siku chache zilizopita waziri Kigoda alizushiwa kifo katika mitandao ya kijamii jambo lililokanushwa vikali na serikali kupitia kwa masemaji wake Bw. Assah Mwambene

Dr. Kigoda ni waziri wa pili kufariki katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu baada ya waziri Celina Kombani naye kufariki dunia mwezi uliopita katika hospitali hiyo hiyo ya Apollo ya India alikokuwa akipatiwa matibabu

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top