Pigo kwa ACT, kampeni zasitishwa baada ya Mgombea Urais kushindwa kuendelea

Kampeni za mgombea urais wa Chama cha ACT-Wazalendo, Anna Mgwhira, zimelazimika kusitishwa mkoani Manyara baada ya daktari wa mgombea huyo kumshauri apumzike kwa muda kufuatia kupatwa na homa ghafla. Mgombea mwenza wa ACT-Wazalendo, Hamad Yusuph, ndiye aliyetoa taarifa hiyo juzi wakati akiwahutubia wananchi wa mjini Babati.

Yusuph alisema, Mghwira ambaye alikuwa wilayani Mbulu, alishindwa kufika Babati kuendelea na mikutano yake kutokana na kukumbwa na homa. Ameamka amechoka sana huku akijisikia homa, hivyo, daktari wake amemshauri apumzike kwa siku moja,î alisema.

Hata hivyo, alisema chama hicho kimejipanga vizuri kuendelea na mikutano mbalimbali kwa kutumia usafiri wa ‘chopa’ ili kukabiliana vizuri na mikikimikiki ambayo imemchosha mgombea wao.

Aidha, aliwaahidi wananchi wa Babati kuwa mgombea huyo atakuja yeye mwenyewe maana wakianza kutumia chopa itakua rahisi.

Wakati huo huo, mgombea mwenza huyo alisema iwapo Watanzania watakipa ridhaa chama chao kushika madaraka ya kuongoza nchi, watarekebisha mikataba yote ya madini ambayo imesainiwa vipindi vyote vya uongozi uliomaliza na unaomaliza muda wake na kushindwa kuwanufaisha wananchi badala yake inakuwa kero kwa wale wanaoishi karibu na migodi.


Chanzo: Nipashe

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top