Umoja wa Ulaya waiasa Tanzania kuhakikisha sheria ya uhalifu wa mtandaoni haikiuki haki za Raia wake

Mkuu wa Umoja wa Ulaya, Mabalozi wa Ubelgiji, Denmark, Ufini, Ufaransa, Ujerumani, Ireland, Italia, Uholanzi, Hispania, Sweden, Uingereza
na Mabalozi wa Canada, Norway, Uswisi na Marekani wanatoa tamko lifuatalo katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mabalozi wa Umoja wa Ulaya, Ubelgiji, Denmark, Ufini, Ufaransa, Ujerumani, Ireland, Italia, Uholanzi, Hispania, Sweden, Uingereza na Mabalozi wa Canada, Norway, Uswisi na Marekani

wanaikumbusha Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuwa ilijizatiti kutumia Sheria ya Uhalifu wa Kimtandao ya 2015 kwa namna ambayo inaheshimu uhuru wa kimsingi na kushughulikia uwezekano wa tafsiri hasi ya sheria hiyo. Hata hivyo, kesi za kwanza za matumizi ya sheria hiyo  zimeongeza wasiwasi katika ukiukwaji wa misingi ya uhuru.

Mabalozi wana wasiwasi kuhusu kukamatwa hivi karibuni kwa wafanyakazi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (Legal and Human Rights Centre) pamoja na vifaa muhimu vya kiufundi, Sehemu ya 16 ya Sheria ya Uhalifu wa mitandao ikitumika kama rejea. Matukio hayo yalitokea wakati shirika hilo lilikuwa likiandaa maoni yaliyotolewa na waangalizi wa uchaguzi nchini kote, kazi ambayo kituo hicho cha haki za binadamu kilipewa kibali na Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Mabalozi wanafahamu kuwa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu ni mwanachama wa Umoja wa Watetezi wa Haki za Binadamu.

Kama ilivyoelekezwa katika Mkataba wa Demokrasia wa Afrika, Uchaguzi na Utawala, Mabalozi wanaamini "kuna haja ya kuimarisha waangalizi wa uchaguzi katika nafasi yao, hasa kwa kuzingatia umuhimu wao katika kuhakiki utaratibu, uwazi na uaminifu wa chaguzi."

Mabalozi wanaisihi Serikali ya Tanzania kuhakikisha utekelezaji wa Sheria ya Uhalifu wa Kimtandao haisababishi uvunjifu wa haki za binadamu na uhuru wa kimsingi, hasa uhuru wa kujieleza na kujumuika na haki ya kushiriki katika chaguzi za uhakika na kwamba inaheshimu misingi ya utawala bora na jukumu la waangalizi wa uchaguzi na mashirika ya kiraia katika michakato ya kidemokrasia.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top