Viongozi wanne wa CDM toka ngazi ya Wilaya na Kata katika Mkoa wa Arusha wameachia nyadhifa zao na kujitoa uanachama wa chama hicho.
Viongozi hao, Amani Torongey (Mwenyekiti Monduli), Revocatus Parapara (Mwenyekiti Ngorongoro), Gerald Majengo (Mwenyekiti Kata ya Terati) na Prosper Mfinanga (Katibu Mwenezi Kata ya Olorien) wamekutana na wanahabari kueleza kuwa wameamua kuwa raia wa kawaida kutokana na kutokupewa fedha za kuendesha chama.
Pia, wamedai kutokuwa na uhuru wa kuchangia hoja wakati wa mikutano mbalimbali na iwapo wakichangia, wakibainika, hufukuzwa katika nyadhifa zao.
Post a Comment