Ajali ya fuso yatokea Shinyanga na kuua na kujeruhi wengine 29

Hapa ni katika eneo la dharura katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga ambapo majeruhi 29 hadi sasa wamepokelewa kufuatia ajali ya gari aina ya fuso iliyokuwa imebeba watu wengi pamoja na mizigo kuelekea katika mnada wa Mhunze uliopo wilayani Kishapu mkoani Shinyanga.
Ajali hiyo imetokea asubuhi ya leo Alhamis.Pichani majeruhi waliendelea kuhudumiwa na wataalam wa afya katika hospotali ya mkoa wa Shinyanga


Kwa mujibu wa kaimu mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Shinyanga Dkt Maguja Daniel  kuwa mpaka sasa wamepokea miili miwili ya marehemu na majeruhi 29
Huduma inaendelea kutolewa katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga

Baadhi ya majeruhi walisema kuwa gari aina ya fuso waliyokuwa wamepanda tena kwa kujazana ilikuwa inafukuzana na fuso nyingine na ghafla walijikuta wakiwa wameshapinduka
Kulia ni kaimu mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Shinyanga Dkt Maguja Daniel akichukua maelezo kutoka kwa askari wa usalama barabarani
Majeruhi akipelekwa wodini
 

Miili ya marehemu ikiwa katika eneo la dharura katika hospitali ya mkoa wa shinyanga

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top