Kwa mijibu wa vyombo ya habari vya Mexico,Mayor wa jiji hilo anaefahamika kwa jina la Joel Vasquez Rojas amefunga ndoa na mamba kama ishara ya kusaidia kuongezeka kwa samaki katika hifadhi ya Pwani ya Pasifiki.
Sherehe ya harusi hii ilifanyika katika ukumbi wa Huamelula,San Pedro kusini mwa Mexico. Wavuvi wengi katika jiji hilo wanaamini mamba ni mfalme na anaweza kuleta mabadiliko mengi katika uvuvi wa baharini.
Wakati wa sherehe bwana harusi alitangaza: "Ni matakwa yake kuoa princess na amemchagua huyo mamba na kula nae kiapo na sasa anajulikana kama "mke" wa Mayor"
Pichani ni mamba akiwa amevalishwa shela nyeupe kuashiri kuwa ni bibi harusi
Post a Comment