Gari lililokuwa limebeba rangi likitokea jijini Dar es salaam kwenda nchi jirani ya Rwanda limepinduka katika mji wa Tinde mkoani Shinyanga majira ya saa 7 mchana leo na kusababisha usumbufu kwa madereva wengine baada ya kukosa sehemu ya kupita hivyo kulazimika kupita njia ya pembeni ambayo ilikuwa ikiwapa usumbufu wakati wa kupishana kutokana na barabara hiyo kuwa nyembamba.
Ajali hiyo haija sababisha madhara kwani wakati inatokea kuikuwa hakuna gari nyingine karibu huku wananchi wakifulika kila mmoja akiwahi kuchota rangi iliyokuwa ikimwagika
Baadhi ya ndoo za rangi zikiwa zimewekwa pembeni ya barabara huku asilimia kubwa zimepasuka.
Dereva wa gari hilo akishuhudia jinsi wananchi wanavyo gombania rangi ilimradi kila mmoja apate chake mapema.
wananchi wakiendelea na zoezi la kuchukuwa rangi iliyomwagika baada ya ajali hiyo kutokea
Tela la gari lililokuwa limebeba rangi likiwa limeanguka katikati ya barabara inayoelekea wilaya ya Kahama na nchi jirani ya Rwanda.
Wananchi wakichangamkia biashara ya rangi iliyokuwa imemwagika ili wakauze ambapo ndoo ya lita 10 sh 10,000 na lita 20 ni sh 20,000
Kila mmoja akiwahi kuchukuwa chake mapema
Tela la gari ambalo limepinduka.
Post a Comment