Rose Ndauka na Chaz Baba ndani ya bifu kali

Ni dhahiri kuwa sasa, staa wa filamu za Kibongo, Rose Ndauka na Rais wa Bendi ya Mashujaa Musica, Charles Gabriel ‘Chaz Baba’ wapo kwenye bifu zito.Habari kutoka kwa paparaziwetu zinasema kuwa, chanzo cha bifu hilo ni fedha, ambapo Rose alikodisha gari la Chaz Baba kwa ajili ya matumizi yake lakini akalirudisha likiwa limeharibika na kumuomba Chaz alitengeneze kisha angemlipa fedha zake, lakini hakufanya hivyo.

“Alikodi gari kwa Chaz, lakini aliporudisha lilikuwa bovu, akamuomba Chaz alitengeze angemlipa, baada ya hapo akaingia mitini. Chaz alikasirika sana, maana hata Rose alipopigiwa simu alikuwa hapokei.
“Imefikia hatua Chaz ametoa kiapo kibaya, amesema hata akifa, maiti yake isizikwe mpaka Rose alipe fedha zake kwanza,” kilitiririka chanzo hicho.
Akizungumzia ishu hiyo, Chaz alisema, kitu alichokifanya Rose si kizuri na kamwe hawezi kumsamehe mpaka amlipe fedha zake.  “Unajua Rose alikuja kwangu na kukodi gari yangu aina ya Toyota Noah, akarudisha likiwa halitamaniki kabisa, nilipomwuliza akasema walipata ajali, nikamtaka akalitengeneze, akasema hana pesa kwa hiyo nitengeneze atanilipa.

“Tangu siku hiyo sijaona simu yake wala meseji, hata nikimpigia hapokei. Nimeingia hasara ya kwenda kutengeneza kwa shilingi laki tano, pesa yangu inaniuma, nataka anilipe.
“Hata kama nikifa leo, maiti yangu isizikwe mpaka Rose alipe haki zangu kwanza. Akitangulia yeye utaratibu utakuwa hivyo sitokubali azikwe hadi ndugu zake wanilipe fedha zangu,” alisema Chaz Baba.
Baada ya kupata habari hiyo kutoka kwa Chaz paparaziwetu alimtafuta Rose kujua kwanini ameshindwa kulipa deni la watu hadi mdai anatoa kiapo kibaya kama kile, akaruka vikali.

“Ni kweli kabisa mimi nilikodi gari ya Chaz nikawa natembelea na ilivyokuja kuharibika nililitengeneza mimi na kwenda kumkabidhi lakini hakuridhika na namna lilivyotengenezwa  ndiyo maana anasema ananidai lakini mimi sijui hilo deni,” alisema Rose.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top