Davido atua Dar kwa ajili ya Fiesta

 Msanii kutoka nchini Nigeria Davido (wa kwanza kutoka kushoto) akiwa sehemu ya VIP na baadhi ya jamaa zake muda mfupi baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere usiku wa kuamkia leo.
Baadhi ya mapaparazi wakiwajibika kupata picha za matukio ya ujio wa Davido kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere muda mfupi baada ya kuwasili akitokea nchini Nigeria.
Mtangazaji wa Clouds TV, Lady Haha (kushotoi), akifanya mahojiano na Davido muda mfupi baada ya kuwasili jijini Dar es Salaam.
Mwandishi wa Habari wa Global Publishers LTD, Musa Mateja (kushoto), akiwa na Davido muda mfupi baada ya kutua jijini Dar es Salaam.
Davido akionyesha tisheti yenye maneno ya kauli mbiu ya tamasha la Serengeti Fiesta 2014, mara baada ya kukabidhiwa na mmoja wa wahusika wa tamasha hilo.
Davido (wa pili kutoka kushoto) akijadiliana jambo na wenzake baada ya kutua kwenye Uwanja wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, usiku wa kuamkia leo.
Davido akizungumza jambo na meneja wake sehemu ya VIP ya Uwanja wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mara baada ya kutua nchini Tanzania.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top