Habari mpya kutoka kwa mastaa wanaodaiwa kuvunjika kwa ndoa yao, Judith Wambura Mbibo ‘Lady Jaydee’ na Gardner G. Habash ‘Kaptaini’, inasemekana wamevunja mkataba wa kuendesha Mgahawa wa Nyumbani Lounge uliopo Ada Estate, Kinondoni jijini Dar.
Mbongo Fleva, Judith Wambura Mbibo ‘Lady Jaydee’. Kwa mujibu wa mtoa habari wetu, wawili hao walidaiwa kufikia uamuzi wa kuvunja mkataba baada ya kuona ndoa yao inasuasua kutokana na migogoro.“Lady Jaydee au Jide alipoona mambo yanakwenda ndivyosivyo alimshauri Gardner wavunje mkataba wa Nyumbani Lounge ili kila mmoja awe na businesses (biashara) zake.
“Walimfuata mmiliki wa jengo, wakamwambia kwamba wanavunja, akawakubalia,” kilinyetisha chanzo makini. Chanzo hicho kilizidi kwenda mbali zaidi na kudai kuwa mgahawa huo kwa sasa unamilikiwa na mzungu.
‘Lady Jaydee’ na Gardner G. Habash ‘Kaptaini’ wakati wakiwa pamoja. “Mgahawa kwa sasa unamilikiwa na Mzungu mmoja ambaye amenunua baadhi ya vitendea kazi walivyokuwa wakivitumia na Jaydee amekuwa akimsaidia mzungu huyo baadhi ya mambo kwa kuwa ni mgeni Bongo ila sasa Nyumbani Lounge itafunguliwa kwa jina jipya la M.O.G na Jaydee atafanya shoo ya ufunguzi kama msanii tu,” kilisema chanzo hicho.

Baada ya kushibishwa maelezo hayo, mwanahabari wetu alimtafuta Jide bila mafanikio lakini Gardner alipopatikana, alijibu kwa kifupi.
“Siwezi kuzungumza chochote katika suala hilo.”
Jide na Gardner wanadaiwa kutengana na kila mmoja akiishi kivyake lakini wenyewe wamekuwa wakikanusha.

Post a Comment