Wazungu wawili wakutwa wamekufa chumbani kwao jijini Dar.

Wazungu wawili ambao ni mume na mke wanaodaiwa kuwa ni raia wa Afrika Kusini, wamekutwa wamekufa chumbani kwao katika nyumba waliyokuwa wakiishi maeneo ya Slipway, Masaki jijini Dar es Salaam Jumatano hii.
Inadaiwa kuwa baada ya kutotokea kazini katika muda wa kawaida, wafanyakazi wenzao walijaribu kupiga simu zao za mikononi, lakini zote zilikuwa zikiita pasipo kupokelewa karibu mchana kutwa na hivyo kuwapa maswali mengi yasiyo na majibu.
Siku iliyofuata, inadaiwa kuwa wafanyakazi wenzao walipojaribu tena kupiga namba hizo, simu zote mbili hazikupatikana
Moja kati ya majeneza yaliyohifadhiwa miili ya marehemu yakitolewa ndani ya chumba hicho.Chanzo cha kuaminika kimeeleza kuwa wawili hao ambao walikuwa wakifanya kazi katika baa iitwayo Mashua iliyo ndani ya Slipway, huku mwanamke, aliyetajwa kwa jina la Hotsan, akiwa ndiye Meneja, walikutwa chumbani kwao wakiwa wamefariki baada ya kutoonekana kazini tokea Jumanne, siku ambayo Watanzania walikuwa wakikumbuka miaka 15 baada ya kifo cha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere. 
Jeneza lingine likitolewa ndani ya chumba hicho. Awali, walihisi huenda wenzao wameamua kuacha kazi baada ya kupata sehemu nyingine, lakini baadaye wakafikia uamuzi wa kuwafuatilia nyumbani kwao ili kujua kilichotokea.

Walipofika, walikuta milango ikiwa imefungwa kwa ndani, kitu kilichowafanya waamini kuwa walikuwa ndani. Kwa kushirikiana na majirani, wafanyakazi hao waliamua kuvunja mlango wa chumba wanacholala wanandoa hao na kuwakuta wakiwa kitandani wamelala, kila mmoja akiwa amegeukia upande wake.

Baada ya kuona tukio hilo la kushtusha, waliamua kuwaita Polisi ambao walipofika na kuiona miili hiyo, waliamua kuwaita wenzao wa kitengo maalum cha uchunguzi (Crime Investigation) ambao baada ya kufika, waliwataka raia na majirani waliokusanyika hapo kukaa mbali ili kuwapisha kufanya uchunguzi. 
Kamanda Suleiman Kova. Askari hao walikaa na miili ya marehemu kwa zaidi ya saa tatu wakiwafanyia uchunguzi na baada ya kukamilika kwa zoezi hili, miili hiyo ilichukuliwa kupelekwa hospitalini Muhimbili.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwataja marehemu kuwa ni Roxxana Hilari na Hainess Hilton William na kwamba uchunguzi zaidi juu ya kilichowaua unaendelea.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top