Diamond avunja record Afrika Kusini baada ya kutwaa tuzo tatu za Channel O

Msanii Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ ametwaa tuzo tatu za Channel O jana usiku nchini Afrika Kusini. Tuzo hizo ni;
Most Gifted new comer,
Most Gifted Afropop na
Most Gifted East
kupitia wimbo wake wa Number One.

Kupitia ukirasa wake wa Facebook Diamond amewashuru sana mashabiki wa wote walio msupport.

"Kiu kweli, haikuwa rahisi kabisa.. lakini kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu na support kubwa mliyonipa iliwezesha Bongo Flavour yetu kuandika historia mpya kwenye ramani ya muziki wa Afrika...Hii inaonyesha ni jinsi gani umoja ni nguvu na pia jinsi gani muziki wetu ukisupportiwa na kupewa kipaumbele unaweza kufika mbali zaidi... Shukrani sana kwa @channeloafrica @channelotv kwa kuniona na kuthamini kipaji changu, My Family, Management, Media zote zilizokuwa zikinisupport, Watangazaji, Wasanii, Wadau na bila kuwasahau wapendwa wangu" - Ameandika Diamond
Diamond Platnumz akipozi baada ya kutwaa tuzo tatu za Channel O jana usiku nchini Afrika Kusini.


Diamond Platnumz akiongea machache baada ya ushindi huo wa kishindo.
Diamond katika pozi na wadau.

Diamond katika pozi na wadau pamoja na mama yake mzazi, Sandra (wa pili kulia).
Diamond (katikati) akiwa na management yake. Kulia ni Said Fella na Babu Tale (kushoto).

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top