Penzi la Wema na Dimpoz, Kunamengi usiyoyajua bofya hapa kuyajua sasa..

Hii ndiyo habari ya mjini, lile penzi linalonadiwa la Mbongo-Fleva, Omary Faraji Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ na mwigizaji Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ limejaa magumashi, ikidaiwa kuwa jamaa huyo kawekwa kama boya tu, nyuma yake kuna kigogo mzito serikalini ndiye anayekula vinono, Risasi Jumamosi limetonywa.
 Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika, Dimpoz ameagizwa na kigogo huyo awe mpenzi kivuli wa Wema ili kuzuga watu wasishtukie mchezo kama yeye ndiye anayesukuma gududumu la malovee kwa Madam.

“Kutokana na unyeti wa kazi yake, jamaa hataki kujitokeza ‘front’ ndiyo maana ameamua kumtumia Dimpoz kama kanyaboya huku yeye akiendelea kula vyake,” kilisema chanzo hicho.Kikizidi kumwaga ubuyu, chanzo hicho kilidai kigogo huyo ndiye anayedhamini safari zote za Wema na Dimpoz nje ya nchi ikiwemo ile ya juzikati nchini Marekani ambayo ilibuma.

“Jamaa ana pesa chafu, amemnunulia Wema viwanja viwili kimoja kipo Tabata na kingine Kigamboni, Dar, ndiye anayemwezesha Wema katika shughuli zake za kila siku.“Kigogo huyo ndiye chanzo cha Wema kummwaga Diamond, alimpotezea kwa sababu ya maslahi zaidi, hata kwenye bethidei ya Wema mwaka jana, kigogo huyo ndiye aliyegharamia vitu kibao hadi kusababisha Diamond ahoji,” kilisema chanzo chetu.

Jitihada za kumsaka kigogo huyo ili azungumzie ishu hiyo hazikuzaa matunda lakini alipotafutwa Dimpoz na kusomewa tuhuma hizo, alijibu:“Watu watambue kuwa uhusiano wangu na Wema upo kwa ajili ya ‘project’ zangu, niacheni please niinjoi maisha yangu kuhusu huyo kigogo muulizeni vizuri Wema mwenyewe,” alisema Dimpoz.

Mwanahabari wetu alipomvutia waya Wema, alijibu kwa kifupi na kukata simu:
“Ujue sasa hivi mimi sitaki malumbano na mtu, najua kila mtu siku hizi anaongea kila anachojisikia, naomba niachwe na maisha yangu, unayoyasema hayana maana,  wanasema kwa sababu hakuna anayemjua mpenzi wangu wa sasa sina muda wa kubishana.”

Hivi karibuni, wakiwa Sauz, Wema na Dimpoz, picha zao wakiwa kimahaba zilivuja mitandaoni hivyo kuibuka gumzo kuwa huenda kwa sasa nao wanatoka.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top