Vurugu kali Bunjumbura-Burundi: Polisi wapambana na waandamanaji wanaompinga Rais Nkurunzinza kugombea Urais tena.......Katiba ya Nchi hairuhusu mihula mitatu



WAPINZANI wa Serikali nchini Burundi, wameitisha maandamano makubwa leo ya kupinga hatua ya Chama Tawala cha CNDD-FDD kumtangaza Rais Pierre Nkurunziza, wa nchi hiyo kuwania mhula wa tatu katika uchaguzi ujao (Katiba ya Nchi hiyo hairuhusu mihula mitatu).

Mkuu wa Chama cha FNL kilichipigwa marufuku nchini humo, Agathon Rwasa, amepinga vikali uamuzi huo na kusema kwamba unaenda kinyume na Katiba ya Burundi.

Rwasa, amesisitiza kuwa, kuteuliwa kwa Rais Nkurunzinza kw aajili yam hula wa tatu utaitumbukiza nchi hiyo katika matatizo makubwa. Rwasa ndiye aliyekuwa mpinzani mkuu wa rais Pierre Nkurunziza katika uchaguzi mkuu wa mwezi Juni, 2010.

Kufuatia hatua hiyo, wapinzani hao wa serikali kwa nyakati tofauti, wameitisha maandamano makubwa leo Aprili 26, 2015 kupinga hatua hiyo ya chama tawala.

Akimtangaza rasmi Rais Nkurunzinza, Mwenyekiti wa Chama Tawala nchini humo, Pascal Nyebenda, aliwataka wapinzani wa serikali kuwa watulivu na kuachana na Rais Nkurunzinza katika masanduku ya kumipigia kura.

Mzozo wa kisiasa unaendelea kutokota nchini humo ambapo taarifa zinaeleza kuwa hivi sasa kumezuka ghasia katika mji wa Bujumbura nchini humo kati ya maafisa wa Polisi na waandamanaji wanaoishtumu serikali kwa kufanya mapinduzi ya kikatiba.

Waandamanaji walirusha mawe na kuchoma matairi huku maafisa wa Polisi wakilazimika kurusha mabomu ya machozi na risasi bandia hewani ambapo ghasia hizo zinafuatia tangazo lililotolewa siku ya Jumamosi kwamba Rais wa Nkurunziza ameteuliwa na chama chake kuwania muhula wa tatu wa urais.Serikali imesema kuwa maandamano hayo si halali.

Kumbukumbu zinaonyesha kwamba maelfu ya raia wa Burundi wamelitoroka taifa hilo katika majuma ya hivi karibuni wakihofia kuongezeka kwa ghasia hizo, huku taifa hilo likijiandaa kwa uchaguzi mnamo mwezi Juni, 2015.

Wakati hayo yakitokea, mrengo wa upinzani nchini humo unaoundwa na vyama 9, Aprili 21, 2015 ulimtangaza Jean de Dieu Mutabazi, kuwa ndiye atayapeperusha bendera yao katika uchaguzi ujao wa rais nchini humo.

Muungano huo unaojulikana kwa jina la Participatory Opposition Coalition in Burundi (COPA), umemteua Mutabazi kuwa mgombea wake katika uchaguzi huo utakaofanyika Juni mwaka huu.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top