Habari iliyotufikia leo hii, kutoka kwa mwanamuziki mkongwe wa RNB nchini, Judith Wambura Mbibo au maarufu kama Lady Jaydee, ni kuhusu kufungwa kwa biashara yake ya Bar na Restaurant aliyokuwa akiifanya kwa takribani mwaka wa nne sasa toka mwaka 2011, bar hyo iliyotambulika zamani kama nyumbani lounge na baadae kubadilishwa jina kuwa Mog bar restaurant .
Msanii huyo alifunguka kupitia ukurusa wake wa Instagram kuwa ifikapo mwisho wa mwezi huu atafunga biashara hiyo na kuahidi kuja na kitu kizuri zaidi baada ya miezi mitatu ijayo, pia alimshukuru mwenye eneo hilo kwa kumpangishia na kumpa ushirikiano mzuri toka aanze kupanga eneo hilo.
Post a Comment