Ray C: Nilikuwa natania kutafuta mume kupitia Instagram.....



Ray C anaweza kuwa amezivunja roho za wanaume zaidi ya 500 waliojipanga mstari kujibu ofa yake aliyoitangaza kwenye Instagram kuwa anatafuta mume.

Ray C ameiambia Bongo5 kuwa mume mwema hatafutwi kwenye mitandao bali huletwa na mwenyezi Mungu.

“Huo ulikuwa utani tu,” amesema Ray C.

“Nilikuwa nataka kuwafurahisha kidogo watu wangu wa Insta. Watu wengi sana, nimepata simu nyingi kweli kweli. Nimepokea zaidi ya simu 500 mpaka saa sita usiku. Kwahiyo nimeona mashabiki wangu bado wapo, wananipenda sana,” amesema.

“Hapana sina mpango wa kuolewa. Mume mwema anatoka kwa Mungu, huwezi kusema unatangaza. Mume mwema anatoka kwa Mungu nikimpata mtasikia, sasa hivi sipo kwenye mahusiano, sina mtu yoyote.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top