Mteule wa
kuwania urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi katika Uchaguzi Mkuu
ujao, John Pombe Magufuli na Katibu Mwenezi wa CCM, Nape NNauye wakipiga
ngoma.
WAKATI
mteule wa Chama Cha Mapinduzi katika Uchaguzi Mkuu ujao, John Pombe
Magufuli akifahamika kama mtu makini kwenye utekelezaji wa majukumu
yake, imethibitika kuwa waziri huyo wa Ujenzi pia ni mkali kwenye
upigaji wa tumba, Risasi Jumamosi linakupa zaidi.
Hali
hiyo imefahamika baada ya gazeti hili kuchimbua matukio mbalimbali
ambayo yamemuonyesha mbunge huyo wa Chato akipiga tumba kwa umahiri
mkubwa kiasi cha kuwaacha hoi watu wengi.
Mathalan,
katika uzinduzi wa daraja la Mbutu, wilayani Nzega mkoa wa Tabora,
uliofanyika Januari 7, 2013, Magufuli alionekana akipiga Tumba wakati
bendi kongwe ya Msondo Ngoma ikitoa burudani katika hafla hiyo, akiwa
sambamba na wanamuziki wa kundi hilo, Shaaban Dede na Hassan Moshi ‘TX
Jr.
Licha
ya siku hiyo, pia kwa nyakati tofauti Magufuli alionyesha umahiri wake
katika kupiga Tumba katika hafla mbalimbali, kama vile wakati wa ziara
ya Rais Jakaya Kikwete mkoani Kagera, alipojiunga na kundi la
uhamasishaji na burudani la chama hicho tawala, kwa kukitendea haki
kifaa hicho cha muziki.
Aidha,
wabunge wawili wa upinzani, John Mnyika (Ubungo) na Halima Mdee wa Kawe,
watakuwa ni mashuhuda wa uhodari wa Magufuli, kwani katika hafla ya
uzinduzi wa barabara ya Msewe- Baruti iliyofanyika miezi michache
iliyopita, mteuliwa huyo wa CCM aliifanya tena shughuli hiyo mbele ya
umati wa wananchi waliohudhuria.
Aidha,
hivi karibuni wakati akitambulishwa kwa wanachama wa chama hicho kama
mgombea wake katika Viwanja vya Zakheem, Mbagala jijini Dar es Salaam,
akiwa pamoja na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, Magufuli pia
alipiga tumba kwa umahiri wa hali ya juu kabla ya kuhutubia mamia ya
wanachama hao.
Mwanamuziki
mmoja kutoka bendi moja kubwa nchini aliyeomba hifadhi ya jina lake,
alisema Magufuli ni mkali na anaweza kuwafunika wapigaji tumba wengi
nchini.
Post a Comment