Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF),Profesa Ibrahim Lipumba amesafiri kutoka jijini Dar es Salaam hadi nchini Burundi kwa shughuli ambazo hazijafahamika wazi.
Profesa Lipumba aliondoka Dar es Salaam, Alhamisi ya Agosti 6 mwaka huu kwa ndege ya shirika la ndege la Rwanda (Rwanda Air), huku ikiwa haijulikani alikoelekea muda mfupi baada ya kutangaza kujiuzulu wadhifa wake wa uenyekiti wa CUF, kwa kile alichodai kutoaminiwa na wenzake ndani ya chama pamoja na kutofautiana mtazamo na msimamo na Viongozi wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA).
Profesa Lipumba aliondoka Dar es Salaam, Alhamisi ya Agosti 6 mwaka huu kwa ndege ya shirika la ndege la Rwanda (Rwanda Air), huku ikiwa haijulikani alikoelekea muda mfupi baada ya kutangaza kujiuzulu wadhifa wake wa uenyekiti wa CUF, kwa kile alichodai kutoaminiwa na wenzake ndani ya chama pamoja na kutofautiana mtazamo na msimamo na Viongozi wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA).
Uchunguzi uliofanywa na mtandao huu tangu kuondoka nchini kwa Profesa Lipumba, umeonyesha kuwapo kwa upotoshaji wa makusudi wa mahali aliko sasa,na kwamba hata kabla ya kuondoka, kulikuwa na jitihada kubwa za kuficha mwelekeo wa safari yake.
Katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere(JNIA) Dar ambapo Lipumba alifika saa saba mchana siku ya alhamisi na kuonwa na baadhi ya watu waliohojiwa na mtandao huu,alifika eneo hilo akiwa amevaa suti ya rangi ya bluu iliyokoza na shati jeupe.
Baadhi ya watu wake wa karibu waliohojiwa kuhusu safari yake hiyo,walieleza kuwa alipanga kusafiri kwa ndege ya shirika la Kenya (Kenya Airways-KQ 485),lakini mashuhuda waliokuwa uwanja wa ndege walieleza kuwa hakusafiri na ndege hiyo.
Mashuhuda hao walieleza kuwa Profesa Lipumba alifika uwanjani hapo akiwa na walinzi wawili na akiwa mwingi wa wasiwasi,huku macho yake yakiwa yameiva kwa wekundu, na aliondoka na ndege ya Rwanda Air saa tisa alasiri.
Taarifa zilizopatikana muda mfupi baada ya kuondoka,zilieleza kuwa alitua Rwanda na baadaye aliruka tena kuelekea Uswisi.Lakini baadaye ilidaiwa kuwa alisalia nchini Rwanda huku ikiwa haijulikani shughuli aliyokuwa akiifanya.
Baadhi ya wanachama wa CUF waliozungumzia kuondoka kwake,walihoji namna safari hiyo ilivyoandaliwa,huku wakihusisha kuwa na msukumo wa wanasiasa wenye nguvu hapa nchini.
Hata hivyo, mtandao huu jana ulithibitishiwa na mmoja wa wanasiasa wenye mtandao mpana wa mawasiliano ndani na nje ya nchi kuwa Profesa Lipumba baada ya kutua uwanja wa ndege wa Rwanda,alisafiri kwa njia ya barabara kuelekea Burundi, ambako hata hivyo haijulikani yuko sehemu gani na anafanya shughuli gani.
Post a Comment