Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, amesema mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), John Magufuli si msafi katika utendaji kazi wake kama inavyoelezwa kwa Watanzania.
Moja ya kigezo kinachotumiwa na Zitto ni madai ya ‘kukwapuliwa’ kwa Sh. bilioni 87 za Wizara ya Ujenzi anayoongoza.
Alisema fedha hizo ni sehemu ya Sh. bilioni 252 za miradi ya umeme, barabara na miradi maalumu zilizokosa maelezo yake kwa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali aliyowahi kuiongoza akiwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema).
Zitto alisema kukosekana kwa fedha hizo ni kiashiria cha kuwapo matumizi mabaya katika wizara iliyoongozwa na Magufuli.

Awaponda UKAWA.
Zitto alivibeza vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kuwa vimepoteza dira baada ya kumpokea Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa kutoka CCM na kumteua kuwa mgombea urais wao.
Alisema Zitto alipinga hoja iliyowahi kutolewa na baadhi ya viongozi wa Ukawa kuhusu ufisadi kuwa ni mfumo na si mtu binafsi.
Zitto alisema ACT-Wazalendo inalenga kujenga siasa mpya nchini zinazojielekeza katika utii wa maadili na kiongozi wa umma kutangaza mali zake hadharani.
Alitoa wito kwa wapiga kura kuwachagua wagombea wa chama hicho kwa madai kuwa vyama vinavyounda Ukawa vina taswira isiyotofautiana na CCM.
Naye Mweyekiti wa chama hicho, Anna Mughwira, alisema chama chake kitakapompitisha rasmi kuwa mgombea ubunge katika jimbo la Singida Mjini, ataelezea namna atakavyofanikisha kuleta mabadiliko na kuharakisha maendeleo.
“Singida iliachwa nyuma kwa maendeleo tangu enzi ya mkoloni…sasa ni lazima tubadilike ili tupate maendeleo,” alisema.
Post a Comment