Mama Regina Lowassa afunguka haya na wanawake wa Sumbawanga leo

Wanawake nchini wametakiwa wasikubali kurubuniwa na maneno maneno wala vitisho kutoka kwa baadhi ya wanasiasa,bali wauone mwaka huu 2015 kama mwaka wa mabadiliko na kuiweka madarakani serikali sahihi,ili iweze kuwawekea mazingira mazuri ya kufanyia biashara zao,na kuwaondoa kwenye adha ya kujifungulia mahali pasipo salama kwa afya zao.
Akiongea na wanawake wa mjini Sumbawanga mkoani Rukwa,mke wa Mgombea urais kupitia chama cha DEMOKRASIA na maendeleo Chadema na UKAWA mheshimiwa Edward Lowassa, Mama Regina Lowassa,amesema wanawake wanapaswa kufanya mabadiliko kupitia masanduku ya kura mwaka huu, ili wapate neema ya kuwa na mazingira mazuri ya kufanyia shughuli zao za kibiashara zisizokuwa na wingi wa kodi na ushuru kama ilivyo hivi sasa,zinazowaletea kero na kuwafanya wasiwe na maendeleo yoyote.

Kwa upande wao baadhi ya wanawake waliohudhuria kikao hicho, wameiomba serikali ya awamu ya tano itakapoingia madarakani,iwaondoe kwenye adha kubwa ya kufanyia shughuli zao za kibiashara kwenye mazingira yenye miundo mbinu mibovu licha ya kulipa kodi na ushuru mbalimbali,pamoja na kuangalia namna ya kuwalipa wenyeviti wa serikali za mitaa posho.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top