Bakharesa ajibu tuhuma za makontena 349 yaliyopita Bandarini bila kulipiwa kodi

Kumekuwa na taarifa zinazosambazwa katika mitandao ya kijamii kuwa kampuni ya Bakhresa inahusika na upotevu wa Makontena 349 yaliyoripotiwa hivi karibuni kuwa yametolewa bandarini bila kulipiwa ushuru. Taarifa hizo zilitolewa na Waziri Mkuu wakati wa ziara yake ya Bandari ya Dar es salaam hivi karibuni.

Uchunguzi wetu umeonyesha kuwa si kweli kuwa kuna makontena yenye bidhaa zilizoingizwa na kampuni hio ama ni miongoni mwa makontena yaliyohusika katika sakata hilo.

 Isipokuwa kumetokea upotevu wa makontena yaliyoingizwa nchini na baadhi ya wafanyabiashara katika eneo la kuhifadhia makontena(ICD) linalomilikiwa na kampuni hiyo la Azam ICD.

Aidha imebainika kuwa kuna uchunguzi unaofanywa na mamlaka ya mapato nchini TRA, huku kukiwa na ushirikiano na uongozi wa Kampuni hiyo (SSB Group of Companies) kuhakikisha wale wote wanaohusika na upotevu huo wanachukuliwa hatua na kodi yote ya serikali inalipwa na wamiliki wote wa makontena yaliyohusika katika upotevu huo wanawajibishwa.


SSB Group of Companies

Corporate Affairs Department

November 29, 2015

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top