Mwanafunzi achinjwa kwa chupa katika Klabu ya Pombe wakinywa Gongo

Mwanafunzi wa kidato cha sita wa Shule ya Sekondari Thaqaafa ya jijini hapa, Amos Kitala (26) ameuawa kwa kuchinjwa kwa kipande cha chupa shingoni kwenye kilabu cha pombe za kienyeji.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Justus Kamugisha alisema tukio hilo lilitokea Machi 19, mwaka huu saa 10 jioni wakati mwanafunzi huyo akigombana na watu wawili kwenye kilabu hicho.

Kamugisha alisema inadaiwa kabla ya kuuawa Kitala alionekana kuwazidi nguvu wagomvi wake na ndipo walipoamua kuchukua chupa, kuivunja na kumkata nayo shingoni na kusababisha atokwe damu nyingi.

Kamgisha alisema wanamshikilia Ramadhan Sima (27) na Omary Philipo (35) kwa tuhuma za mauaji hayo.

Wakati huohuo; kibarua amekufa kwa kudondoka kutoka kwenye lori alilokuwa akining’inia wakati akidai ujira wa Sh10,000 kwa kupakia kokoto.

Kamugisha alimtaja kibarua aliyepoteza maisha baada ya kudondoka kwa kile kilichodaiwa ni kusukumwa na dereva wa lori hilo aina ya Scania kuwa ni Mashaka Mathias (34), mkazi wa Isamilo.

Dereva huyo, Haji Juma (38) anashikiliwa na polisi kwa mahojiano kuhusiana na kifo cha kibarua huyo.

Katika tukio jingine; Christopher Starabu (34), amefariki dunia baada ya kugongwa na gari wakati akivuka barabara katika eneo la Mabatini.

Kwa mujibu wa Kamugisha, dereva wa gari hilo, Rajabu Mika (30, Mkazi wa Bwiru anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za mauaji hayo.

Mwalimu wa Shule ya Msingi Ilula, John Sinega (29), amefariki dunia baada ya kugongwa gari wakati akiendesha pikipiki.

Kamanda huyo alisema, dereva wa gari hilo, Ismail Jamal (36), anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kusababisha kifo cha mwalimu huyo.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top