Bilionea anayetaka kuinunua Simba, ametaja kilichomsikitisha katika mkutano wa Simba

Siku moja baada ya mkutano mkuu wa Simba kufanyika na kukubali kupitisha maadhimio ya mabadiliko ya kiuongozi ili klabu iendeshwe kwa mfumo wa hisa, bilionea wa 21 Afrika ambaye pia ni mkurugenzi mtendaji wa makampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL) Mohammed Dewji ameelezwa kusikitisha na taarifa za upotoshwaji.

Mohammed Dewji amesikitishwa kutokana na taarifa zilizotolewa katika mkutano mkuu Simba uliofanyika jana July 31 2016, kuwa yeye ambaye aliomba kununua asilimia 51 ya hisa za Simba kama mfumo ukibadilishwa, hajaandika barua kwa uongozi wala kukutana nao ila amekuwa akiongea kupitia vyombo vya habari kitu ambacho sio kweli.

“Kiukweli nimesikitishwa kwa wanaosema dhamira yangu ya kutaka hisa Simba nimeomba kupitia vyombo vya habari na wala sijaandika barua, ukweli nimekutana na Rais wa Simba Evans Aveva zaidi ya mara tatu, ameshakuja ofisi kwangu zaidi ya mara tatu”

“Kuhusu kuandika barua nilikuwa sijaandika kwa sababu mfumo wa hisa niliokuwa nahitaji ulikuwa haupo sasa utaombaje kitu ambacho hakipo, ila leo baada ya mkutano mkuu kukubali nimeandika barua rasmi kwenda kwa uongozi wa Simba na tayari tumeshaituma”

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top