Mume ajilipua kwa petroli Morogoro, Kisa wivu wa Mapenzi

Wivu wa mapenzi? Kigogo mmoja wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa mkoani hapa ambaye ni bosi wa kitengo cha manunuzi, Jackson Maghembe, anadaiwa kutaka kulipua nyumba anayoishi mkewe, Cesilia Njuli kisha kuishia kujilipua mwenyewe.

Tukio hilo lilijiri wiki iliyopita Mtaa wa Kilosa Town Kata ya Mkwatani-Manzese A wilayani Kilosa baada ya wawili hao kuhudhuria kwenye shoo ya Mwanamuziki Aisha Ramadhani ‘Isha Mashauzi’ iliyofanyika katika Ukumbi wa Bablon.

Kwa mujibu wa mashuhuda wetu, wakiwa kwenye shoo hiyo, Maghembe alidaiwa kumpiga mkewe na baadaye kwenda nyumbani kuunguza nyumba hiyo kwa petroli huku watoto wao wawili na mfanyakazi wa ndani wakiwa usingizini.

“Huyu mume wangu nimezaa naye watoto wawili, mwezi wa nne nilimpeleka polisi kwa mara ya tatu ambako tulikubaliana tuachane na tukatiliana saini kwenye jalada lililofunguliwa namba KL\LR\390\2016.

“Baada ya pale, kila mmoja akawa anaishi kwenye nyumba yake na mimi nikawa ninaishi na wanangu.

“Wiki iliyopita nilikwenda kwenye shoo ya Mashauzi kupoteza mawazo. Nikiwa pale ukumbini, yule mume wangu alikuja na kuniomba tucheze wote.

“Kwa kumheshimu kama baba wa watoto wangu nilikubali. Cha ajabu muziki ulipokwisha alining’ang’ania nikalale kwake. Nilimkatalia ndipo akaning’oa wigi kichwani na kunipiga.

“Baada ya kutoka pale ukumbini alikwenda kununua petroli akaimwaga madirishani kwa lengo la kuichoma moto nyumba huku wanaye na msichana wangu wa kazi wakiwa wamelala.

“Wakati akimwaga petroli ilimlowanisha nguo zake hivyo alipowasha kibiriti nyumba iliungua na moto mwingine ulinasa kwenye nguo zake na kumuunguza vibaya.

“Majirani walipofika kwa kushirikiana na mpangaji wangu, Ayoub Paul na msichana wangu wa kazi, Esther Jonas waliwaondoa wanangu na kuhangaika kuuzima moto.

“Kwa sasa yupo hoi Hospitali ya Kilosa kutokana na hali yake kuwa mbaya.”

Hata hivyo, mke huyo ambaye ni nesi wa Hospitali ya Wilaya ya Kilosa alikwenda kumfungulia mumewe huyo jalada la kesi namba KL\ RB\1141\2016 –SHAMBULIO LA KUDHURU MWILI NA UHARIBIFU WA MALI huku madaktari wa hospitali hiyo wakieleza kuwa hali ya jamaa huyo bado ni tete.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top