Mwanaume aota matiti baada ya kuiba Ng'ombe..

Acry Chinhivi Shayamano (40) kutoka  Nherera Mhondoro, Zimbabwe ameota matiti ghafla baada ya kutuhumiwa kuiba ng’ombe na hivyo matiti ni adhabu kutoka kwa mmiliki wa ng’ombe hao. Shayamano alikiri kuwa yeye ni mwizi lakini alikataa kabisa kama aliiba ng’ombe.
“Nani kawaambia nimeota matiti. mimi yangu sio mabaya sana, sijawahi iba ng’ombe yoyote”.
“Ndio niliiba lakini sio ng’ombe. Niliiba DVD na nikakamatwa na kulipa faini” alisema
Acry aliendelea kwa kusema, Bibi yake alipoteza ng’ombe wawili mwezi Februari na ni kipindi hicho ndipo na me niligundua naanza kuotwa na matiti. Watu wakaanza kuonganisha matukio wakati si kweli.
Acry amesema kwamba matiti hayo hayaumi lakini bado yanaendelea kukua na pia akasema inawezekana ni madhara ya dawa za upungufu wa kinga mwilini (ARV) alizokuwa anatumia kwa kipindi cha miaka mitatu sasa.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top