15 wahukumiwa kunyongwa China.........Soma zaidi hapa

www.paparaziwetu.blogspot.com
Matukio ya kukamatwa kwa Watanzania nchini China kwa kesi za biashara ya dawa za kulevya yana idadi kubwa sana ndani ya hii miaka mitano iliyopita.
Miezi miwili iliyopita Balozi wa Tanzania China alithibitisha kwenye  kwamba Watanzania wasiozidi mia mbili ndio wamefungwa kwenye magereza mbalimbali ya China kutokana na kesi tofautitofauti ila dawa za kulevya ndio zinaongoza’
Balozi huyu alisema kwa wakati huo hakuwa na rekodi yoyote ya Mtanzania kuhukumiwa kunyongwa au yeyote ambae tayari ameshanyongwa na kwamba kwa taarifa zaidi Wizara ya mambo ya nje itafutwe.
Baada ya hayo yote, hatimae katibu mkuu wa wizara ya mambo ya nje John Haule March 25 2014 ametaja jumla ya Watanzania waliokamatwa kwa kesi ya dawa za kulevya kwa kusema‘tuna Watanzania wengi tu ambao wapo kwenye magereza kule China japo tumeshindwa kwa harakaharaka kupata idadi ya waliojihusisha na shughuli ya dawa za kulevya.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top