Angalia picha za shilole na mpenzi wake mpya wakila raha

KWA mara nyingine, staa anayekimbiza kwenye filamu na muziki wa mduara, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ au ‘Shishi’ ameibuka katika penzi jipya na bwana mdogo anayechipukia katika muziki wa Bongo Fleva, Nouh Mziwanda, Risasi Mchanganyiko limeinasa.

Kwa mujibu wa paparaziwetu, Shilole kwa sasa hasikii wala haoni kwa Nouh pamoja na kwamba wawili hao wanaonekana kuwa na tofauti kubwa ya kiumri , Shilole akionekana kuwa mkubwa zaidi ya Nouh.


“Shilole ni kama anambemenda  Nouh lakini ndiyo hivyo, haoni wala hasikii, kila siku wako pamoja kama kumbikumbi,” kilisema chanzo chetu.
Paparaziwetu aliwafuatilia wawili hao kwa nyakati tofauti na kufanikiwa kuzinasa picha zao walizozipiga katika mikao ya kimahaba.Baada ya kuzinasa picha hizo, paparaziwetu alimtafuta  Nouh na kumweka mtu kati kuhusu uhusiano wake na Shilole. 
www.paparaziwetu.blogspot.com


“Ni kweli ninatoka na Shilole ni mpenzi wangu na sidhani kama nitakuja kuachana naye maana tunapendana sana na nimevutiwa na mavituz yake,” alisema Nouh. Kuhusu tofauti ya umri wake na ule wa Shilole, Nouh alisema umri huwa haumati katika mapenzi.

“Mapenzi ni mapenzi na umri utabaki kuwa namba tu, ni vyema  mtu ukaongozwa na hisia zako kuliko kuhofia umri wa mtu ndiyo maana miye ninakula vinono,” alisisitiza. Pia, Nouh alisema hakutarajia kukubaliwa na  Shilole baada ya kumtokea walipokutana  katika  studio moja jijni Dar na sasa wamekolea kwenye penzi motomoto.


“Nampenda Shishi, nafanya kila njia nimshawishi awe mke wangu wa ndoa,” aliongeza. Hata hivyo, Shilole alipozungumza na paparaziwetu alipatwa na  kigugumizi kukubali uhusiano wake wa kimapenzi na kinda huyo wa Bongo Fleva.

Shilole alisema Nouh ni rafiki yake kama walivyo marafiki zake wengine.
paparaziwetu alipomuonesha picha zao walizokuwa wamekaa katika mikao ya  kihasarahasara, Shilole aliangua kicheko na kisha akasema: “Mh! Sina la kuwajibu kama picha zinasema mimi na Nouh ni wapenzi haya.”


Hii siyo mara ya kwanza kwa Shilole kuripotiwa kutoka na Serengeti Boy, siku za nyuma alishawahi kuripotiwa na gazeti dada na hili la Ijumaa Wikienda akisema anapenda kutoka na ‘Serengeti Boys’.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top