Maamuzi ya kura ya WAZI au ya SIRI, Bungeni Dodoma leo

Wapendwa  wasomaji, kama Mwenyekiti wa Bunge Maalum, Sammuel Sitta alivyotangaza jana wakati akiahirisha kikao cha jioni, kwamba, kazi kubwa ya leo ni kufanya maamuzi juu ya vifungu vya 37 na 38 vya Kanuni za Bunge Maalum ambavyo vinahusu jinsi ya kufanya maamuzi. Mjadala hapa ambao umeteka hisia za wananchi wengi ndani na nje ya Bunge ni juu ya Kura ya Siri au ya Wazi.

Hakika tumeshuhudia mjadala mkali ambapo kila kundi likijitahidi kutetea msimamo wake. Ninapozungumzia makundi nina maana ya CCM kwa upande mmoja ambapo idadi kubwa ya wabunge wake wanaunga mkono Kura ya Wazi na wabunge wa vyama vya Upinzani kwa Upande mwingine ambao wengi wao wanaunga mkono Kura ya Siri.

 Aidha, katika jitihada hizo za kutetea misimamo yao, baadhi ya wabunge walijikuta wakivuka mipaka ya kuongea kwa kutoa lugha zisizo za staha na hivyo kulazimishwa kuondoa kauli zao na kuomba radhi. Hata hivyo, kwa vile Kamati ya Kanuni imeamua kuwa aina zote za kura zitatumika katika kufanya maamuzi, ni wazi kuwa suala hili ni kama limemalizika.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti, ni kwamba leo hakutakuwa na mjadala wowote bali yatafanywa maamuzi ili kujua ni aina gani ya kura itatumika. Wakati akiahirisha kikao cha jana, Mwenyekiti alitangaza majina ya wabunge wanaounda Kamati ya Muda ya Mashauriano ambao walikutana jana kujadili masuala mbalimbali likiwemo suala la Kura ya Siri na Wazi. Ni imani ya Watanzania wengi kwamba kikao hicho kimeleta suluhu muafaka katika jambo hilo.


Michango  ya  wabunge
Wabunge wameendelea kuchangia juu ya mapendekezo ya Kamati ya Kanuni. Mwenyekiti amesema kuwa ataruhusu wabunge wachache wachangie.

Amesema kuwa kuna wachangiaji zaidi ya 100 hivyo kwa idadi hiyo hawawezi kuongea wote. Pia kwa kuwa ni ama kura za wazi ama siri, ni wazi kuwa hakutakuwa na mawazo mbadala wa hoja hizo.

  Shaka Hamisi Shaka
Shaka Hamisi Shaka sasa anaongea. Anaanza kwa kuunga mkono hoja ya Kamati. Yeye anasema kuwa ni muumini wa kura za wazi na anawaasa waumini wa uwazi kupiga kura za wazi ili kuzuia yale yaliyotokea mwaka 1984 kule Zanzibar. Anawaasa wabunge kujadili kwa hoja badala ya kushambulia vyama vya siasa.

Dianna Chilolo
Dianna Chilolo amesema kuwa mifumo yote inaweza kutumika kufanya maamuzi. Amesema kuwa yeye ni muumini wa kura ya wazi hivyo anamuomba mwenyekiti kufunga mjadala ili maamuzi yafanyike.
 
Mheshimiwa Chombo
Anayeongea sasa ni Mheshimiwa Chombo. Anasema kuwa yeye ni muumini wa kura ya wazi. Hata hivyo anasemamkuwa kwa vile Kamati imependekeza mifumo yote miwili, haoni sababu ya watu kulumbana kwenye hoja hizo.

 Anawashangaa wale wanaopinga mfumo uliopendekezwa na Kamati eti kwa vile haujawahi kutumika. Anasema kuwa hata Tanzania ilipoanzisha mfumo wa serikali mbili, mfumo huo ulikuwa haujawahi kutumiwa mahala popote. Kwamba Tanzania ndiyo ilikuwa ya kwanza kutumia aina hiyo ya muungano hivyo si vibaya tukiwa wa kwanza kutumia mfumo wa kura ya wazi na siri kwa wakati mmoja.

 Jesca Msavatavangu
Jesca Msavatavangu anaunga mkono maamuzi ya kamati. Kwamba uamuzi huo ni mzuri kwa vile hakuna aliye tayari kusacrifice msimamo wake.

Pia anasema kuwa kuna majungu yameanza kujitokeza hasa juu ya takrima. Anasema kuwa inapotokea kiongozi wa ccm anapowaalika wabunge wa 201 inakuwa nongwa. Ila viongozi wa UKAWA walipowaalika wabunge hao chini ya mwenyekiti wa UKAWA Freeman Mbowe inakuwa sawa. Anasema kuwa ikiwa watapiga kura ya wazi, unafiki utaondoka.
 
Medeye
Sasa anaongea aole Medeye. Kwanza anapongeza maneno ya Askofu Donald Mtetemela ambaye amekemea maneno mabaya na yanayochukiza. Anaipongeza Kamati ya Kanuni kwa maamuzi waliyofanya.

Anasema kuwa Tanzania haitakuwa ya kwanza kufanya hivyo. Anasema kuwa mwaka 1964 wakati shirika la posta duniani walipotaka kuifukuza Afrika ya Kusini walitumia kura ya Siri na Wazi. Bunge la Italia linarumia kura ya siri na wazi tangu miaka ya 1970.

Kwa upande wake, anapendekeza wapige kura ya kuamua kutumia kati ya kura hizo mbili. Pia anapendekeza mfumo mwingine ambapo wabunge watapiga kwanza kura ya wazi na hatimaye wabunge hao hao watapiga kura ya siri. Kwamba deciding vote itakuwa ni ile kura ya siri.
 
Pauline Gekul
Pauline Gekul anasema kuwa yeye ni muumini wa kura ya siri. Pia ana wasiwasi wa namna ya upigaji kura. Kwamba huku kura za wazi zinapigwa, kule kura ya siri inapigwa. Kwa hali hiyo anasema kuwa itawachanganya sana.

Pia anawashangaa wale wanaosema kuwa wapinzani hawataki katiba. Anasema kuwa ni wapinzani ndio walioshinikiza serikali hadi mchakato wa kariba mpya.

Pia anasema kuwa ccm inataka mfumo wa kura ya wazi kwa lengo ka kuwadhibiti wanaodai atanganyika. Yeye anasema kuwa ni vema maamuzi yakafanywa ili aina moja tu ya kura itumike kufanya maamuzi.

Paul Lwanji
Paul Lwanji anasema kuwa yeye ni muumini wa kura ya wazi. Anasema kuwa wanaopendekeza kuranya siri wana ajenda ya siri. Anasema kuwa kuna wachache wanataka kuharibu amani ya nchi hii kupitia mchakato huu wa katiba baada ya kushindwa kwenye uchaguzi.

Anasema kuwa tuhuma zinazopikwa ili kuhalalisha kura ya siri anasema si za kweli. Hata hivyo anasema kuwa kwa vile kamati imeamua, ni wazi kuwa maamuzi hayo ya kamati yameletwa kwa lengo la kujenga muafaka.
 
Said Arfi
Said Arfi anasema maamuzi ya kuwa na kura za aina mbili yaani siri na wazi hayawezi kutufikisha popote. Pia anasema wakati wa kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi, wengi walikataa na wachache wakakubali, lakini kutokana na hekima, maoni ya wachache yalifuatwa.

 Anasema kuwa kitendo cha kutumia mifumo yote miwili ni wazi kuwa italeta balqq huko mbele. Anatolea mfano kuwa huwezi kuendesha gari toka Dar Hadi Dodoma katikati ya barabara. Anasema kuwa kwa kufanya hivyo ni wazi utasababisha ajali. Anawataka CCM kuwakubalia wachache kwa kuunga mkono kura ya siri kwa lengo la kulinusuru taifa.
 
Mheshimiwa Mashimba
Mheshimiwa Mashimba anasema kuwa suala hili limeisha kwa vile linatoa uhuru kwa kila mtu. Hivyo anamtaka mwenyekiti kufanya maamuzi juu ya suala hilo. Anaunga mkono maamuzi ya Kamati ya Kanuni.
 
Selemani Jafo
Selemani Jafo anasema kuwa mapendekezo ya Kamati ni mazuri kwa vile yanatoa uhuru wa wabunge kuamua. Anamtaka mwenyekiti kuamua juu ya jambo hili.

Lisper Miguma
- Lisper Miguma anachangia sasa. Anashangaa mgawanyiko uliojitokeza juu ya jambo hili. Anashangaa maamuzi ya kamati ya kupendekeza mifumomyote miwili. Yeye mtazamo wake kuwa mapendekezo hayo ni hatari kwa usalama wao.

 Yeye anapendekeza kura ya siri na wazi itumike kulingana na uzito wa vifungu.Pia ameunga mkono mapendekezo ya wabunge wote kupiga kura zote wakianza na kura ya wazi na kumalizia kura ya siri.

Maelezo ya Wajumbe wa kamati ndogo ya Maridhiano

John Mnyika
- Michango ya wabunge imemalizika na sasa ni maelezo ya wajumbe wa kamati ndogo ya maridhiano. Anayeongea sasa ni John Mnyika. Anasema kuwa mazungumzo waliyofanya yamesaidia kusonga mbele ingawa wamekubaliana kutokubaliana.

 Anasema kuwa walivutana sana juu jambo hilo. Kutokana na hali hiyo, walikubaliana kuwa maamuzi hayo yafanywe kwa kura. Kwamba wabunge waamue kupiga ama kura ya siri ama ya wazi na maamuzi hayo yaheshimike na watu wote. Makubaliano yaliyofikiwa ni kwamba Wapinzani watapiga kura ya hapana na wale wa CCM watapiga kura ya ndiyo.

Aidha anasema kuwa wao kama wapinzani hawana nia ya kukwamisha mchakato huo. Anasema kuwa wao kama wapinzani walikuwa wa kwanza kumshawishi Rais aanzishe mchakato wa katiba mpya. Pia amemuomba Waziri Mkuu kumfikishia salamu Rais ambaye amenukuliwa akisema kuwa katiba ya zamani itaendelea kutumika ikiwa mchakato wamkariba mpya utakwama.

 Anasema kuwa wao kama wapinzani watahakikisha kuwa katiba mpya inapatikana na hawapo tayari mkuendelea kutumia katiba ya zamani wakati wqnq uwezo wa kupata katiba mpya.

Ibrahimu Lipumba
 Ibrahimu Lipumba anaanza kwa kuwaomba radhi wabunge wa 201 kwa kukwazika na mjadala wa jana. Kuhusu maamuzi ya kamati ya kanuni anasema kuwa hakika CCM imekuwa na msimamo mkubwa juu ya jambo hilo.

Kwa vile wao wapo wengi, wapinzani wameamua kukubaliana kuwa jambo hili lifike mwisho kwa kufanya maamuzi. Yeye anapendekeza kura moja tu itumike kuamua juu ya jambo hilo. Pia amewaomba CCM kupunguza misimamo yao kwa lengo la kusonga mbele.

Vuai Ali Vuai
Vuai Ali Vuai anasema kuwa jambo hili lilikuwa na mvutano mkubwa. Ila anasema kuwa wao kama CCM wamesema kuwa wameamua kwenda na kura zote yaani siri na wazi.

Anasema kuwa wakati wa majadiliano, wapinzani walikuwa wanasema kuwa CCM hawapo tayari kuendelea na mchakato wa katiba. Hata hivyo yeye alijibu kuwa CCM ITAKUWA YA MWISHO kujitoa kwenye mchakato huo. Pia waliambiwa kuwa CCM ni watukutu na hawataki kuachia kila kitu. Ila yeye alijibu kuwa CCM ni wasikivu na wamekuwa wakieidhia mambo mengi tangu mchakato huu ulipoanza. Kutokana na hali hiyo, ndipo walipoamua kuwa kura zote zitumike katika kufanya maamuzi.

 Anawashukuru viongozi wa dini kwa msaada mkubwa walioutoa wakati wa majadiliano. Pia anawapongeza wabunge wa kundi la 201 kwa uvumilivu waliouonesha wakati wote licha ya shutuma wanazopewa.


Askofu Donald Mtetemela
Baba Askofu Donald Mtetemela anaongea kwa niaba ya viongozi wa dini. Anasema kuwa kutofautiana binadamu ni jambo la kawaida.

Hata hivyo anasema kuwa wakati mwingine waru huachia misimamo yao kwa lengo la kusonga mbele. Ni kutokana na hali hiyo ndipo wabunge wa CCM na vyama vingine walipoamua kukubaliana kutumia njia zote yaani kura ya siri na wazi kwa lengo la kusonga mbele.

 Anasema kuwa wametumia siku 40 kutunga kanuni kabla ya hata ya kuanza kujadili Rasimu ya Katiba. Anasema kuwa kwa vile siku ya Ijumaa, Jumamosi ja Jumapili ni siku za Ibada, ni wazi kuwa wabunge wataendelea kuomba kwa lengo la kusonga mbele.


 Mwenyekiti Kificho
>>>Sasa Mwenyekiti wa Kamati ya Kanuni anaitwa kutoa ufafanuzi wa juu ya njia gani itumike kufanya maamuzi ya vifungu hivyo. Mwenyekiti Kificho anasema kuwa maamuzi yaliyofikiwa ya kutumia kura zoye ya siri na wazi yatatumika wakati wa kupitisha vifungu vya kanuni. Anasema kuwa utaratibu uliotumika kupitisha vifungu vingine vya kanuni utumike.

Hata hivyo, Ibrahimu Lipumba anasema kuwa walikubaliana kupiga kura ya siri kuamua jambo hilo. Mwenyekiti wa abunge Maalum, Sammuel Sitta anasema kuwa maamuzi yaliyofikiwa wakati wa mashauriano ndiyo yatakayofikia kufanya maamuzi.

 Kutokana na hali hiyo, kura ya Siri itatumika kufanya maamuzi juu  ya mapendekezo ya kamati ya kanuni. Katika hili wasomaji ni kwamba kura inayopigwa ni ya kuamua kuridhia au kutoridhia maamuzi ya kamati ya kanuni juu ya vifungu vya 37 na 38.


   Prof Costa Mahalu
Prof Costa Mahalu kwa niaba ya Mwenyekiti wa Kamati ya Kanuni ameitwa kuleta ufafanuzi juu ya mapendekezo ya Kamati ya Kanuni kuhusu kanuni za 37 na 38. Anasema kuwa kamati ya kanuni wamepokea hoja kutoka kwa John Mnyika.

 Anasema kuwa mapendekezo ya Mnyika yalilenga kufanya marekebisho ya mapendekezonya kanuni. Katika hilo anasema kuwa wameshindwa kulifanyia marekebisho kwa vile kanuni zilizopo hazina muongozo juu ya jambo hilo.

Pili anasema kuwa John Mnyika alileta marekebisho juu ya kanuni ya 38. Hata hivyo anasema kuwa pendekezo hilo wameshindwa kulifanyia kazi kwa vile Mnyika ameshindwa kutoa sababu za kuleta mapendekezo hayo.

 Ole Nasha
Ole Nasha anaongea kwa niaba ya kura ya kielectronic. Anasema kuwa, walipopata hoja hiyo waliwasiliana na ofisi ya katibu wa bunge. Anasema kuwa baada ya kuwasiliana na ofisi ya katibu wa bunge, walifanya majaribio na ukaonekana kuwa ungeweza kufaa. Hata hivyo anasema kuwa kwa vile ni mfumo wa kielectronic, unaweza kuingiliwa na ukatoa majibu yasiyo sahihi.

 Pia anasema kuwa kwa vile ni mashine zinazotumiwa, zinaweza kuharibika wakati wowote na hivyo kuvuruga mfumo mzima. Pia anasema kuwa matatizo yaliyojitokeza kule Kenya kwenye uchaguzi mkuu uliopita imekuwa ni somo kwao.

Pia anasema kuwa kutokana na hali ya kutoaminiana, waliona kuwa mfumom huo usingefaa. Kutokana na hali hiyo, waliamua kuwa mfumo huo usitumike.

 Evod Mmanda
Evod Mmanda naye ameitwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kanuni kutoa ufafanuzi. Anasema kuwa waliamua kutumia mifumo yote miwili kutokana na kuibuka makundi mawili yanayopenda kura ya wazi na siri.

 Hivyo ili kutoa uhuru kwa makundi yote ndipo walipoamua kutumia mfumo uliopendekezwa. Alisema pia kuwa mapendekezo yao yamezingatia kanuni mbalimbali za bunge maalum ikiwemo kanuninya 39 (3).

 Mbatia
Mwenyekiti wa Kamati ya Kanuni amemuita James Mbatia kuongea. Mbatia anasemam kuwa Kamati za Maridhiano zifikie maridhiano ya kweli. Pia amewataka wajumbe walinde hadhi ya wqbunge wenzao hasa katika kujadili hoja.amewaomba wabunge kuchunga ndimi zao ili wasikwaze wengine.

 Amewaomba radhi wabunge wa kundi la 201 kutokana na kukwazika na mjadala wa jana. Ametumia  muda huo kuomba radhi kwa niaba ya waliokosea ili wasonge mbele.

 Mwenyekiti Kificho  tena
Sasa ameitwa mtoa hoja kuhitimisha hoja yake. Mwenyekiti Kificho anaanza kwa kumshukuru Mwenyekiti.Anasema kuwa wabunge 41 walichangia kwa kuongea na 2 walichangia kwa maandiahi. Anasema kuwa hoja hii imekuwa na mvutano mkubwa tangu walipoanza kupitisha kanuni.

 Hata mjadala wa jana anasema kuwa ulitawaliwa na uwazi na usiri. Kutokana na hali hiyo ndipo walipoamua kuleta mapendekezo ya kutumia mifumom yote kutegemeana na imani ya mpigaji mkura. Kificho pia anawashukuru wajumbe wote kwa michango yao. Anasema michango imegawanyika makundi manne

    1 Wametaka kura ya wazi na kukataa siri
    2 wametaka siri bila kukubali kura ya wazi
    3 kuna wanaopendekeza matumizi ya kura ya wazi na siri kutegemeana na     uzito wa ibara
    4 Wanaopendekeza matumizi ya mifumo yote

kutokana na hali hiyo, ndipo walipoamua kutumia njia zote. Mwenyekiti Kificho amewasilisha hoja

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top