Kajala aongwa gari na kigogo........Soma hapa

Kajala Masanja.

NI madai mazito! Kwamba, nyota wa muvi za Kibongo, Kajala Masanja amehongwa gari na mtu anayedaiwa kuwa ni kigogo wa Ikulu. Hii ndiyo habari ya mjini kwa sasa na Risasi Jumamosi limeifukunyua.
Kwa mujibu wa habari hizo ambazo zipo hadi kwenye mitandao ya kijamii, hasa Instagram, Kajala alinunuliwa gari hilo aina ya Toyota Brevis lenye rangi ya bluu iliyoiva wiki mbili zilizopita mara baada ya kutua Bongo akitokea nchini China ambako alikwenda kwa mambo yake binafsi.
Brevis aina ya gari aliyonunuliwa Kajala.

Kigogo huyo wa Ikulu ni yule Clement ambaye amewahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi wa Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu.“Mmeisikia hii? Kajala amenunuliwa gari na Kile (Clement), lina thamani ya shilingi milioni kumi na moja, Wema alie tu nakwambia. We ukisema cha nini wenzako wanajiuliza watakipata lini?
 

Muonekano wa ndani wa gari aina ya Brevis.
 
“Kwanza mnajua kama bifu la Wema na Kajala lilitokana na Clement? Alipoachana na Wema akatua kwa msichana anaitwa Naima, lakini akaona bado akaenda hadi kwa Kajala. Wema alipogundua ndiyo akamnunia na kuanza ushoga na Aunt Ezekiel,” msambaza habari za mjini mmoja aliliambia Risasi Jumamosi juzi.
Akaendelea: “Unajua nini? Naamini Wema alimwacha yule bwana na akurudi kwa Diamond baada ya kuona mambo yake siyo mazuri, lakini sasa jamaa (kigogo wa Ikulu) mambo ni safi kwa hiyo anataka kumwoneshea Wema ndiyo maana ameamua kumnunulia gari Kajala baada ya kuwa naye.”
Kajala: “Mimi nimelinunua hili gari kwa mtu. Aliniuzia kwa shilingi milioni kumi na moja (11,000,000). Sijahongwa wala sijanunuliwa. Kuna watu wanataka kunichafua tu.Kuhusu kufa kwa ushoga wao, awali Kajala hakutaka kulizungumzia suala hilo lakini alipobanwa alidai hana tatizo na Wema na kwamba kwa sasa yuko bize kutengeneza filamu zake.

Kwa upande wake, Wema alipopigiwa simu hakupokea lakini siku za nyuma aliwahi kuanika kwamba haamini kama Kajala anaweza kutembea na Clement. Hapo ni wakati ule wakiwa mashoga.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top