Manchester united wamaibuka na ushindi 4-1 dhidi ya Aston Villa

Furaha imerudi katika nafsi ya kocha David Moyes kufuatia Manchester United kuifunga mabao 4-1 Aston Villa Uwanja wa Old Trafford jioni hii katika mchezo wa Ligi Kuu ya England.
Mabao mawili yaliyofungwa na Wayne Rooney dakika za 20 na 45 kwa penalti na mengine ya Juan Mata dakika ya 57 na Javier Hernandez dakika ya 90 yalitosha kuiongezea pointi United.
Villa ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa na Ashley Westwood dakika ya 13 kwa mpira wa adhabu.
Kwa ushindi huu United  inatimiza pointi 54 baada ya kucheza mechi 32 na inaendelea kubaki nafasi yake ile ile ya saba.
 Juan Mata akipambana na Bacuna 
 Rooney akifunga goli kwa penati.
 Kocha David Moyes akisaini karatasi za mashabiki baada ya ushindi leo
 Sir Ferguson akishuhudia mechi ya leo ambayo Man United wameibuka mabingwa dhidi ya Aston Villa.

Kikosi cha Manchester United: De Gea 6, Rafael 5 (Carrick, 45), Jones 6, Vidic 7, Buttner 6; Fletcher 7, Fellaini 6; Kagawa 8 (Januzaj, 67), Mata 7, Young 5; Rooney 8 (Hernandez, 74).

Kikosi cha Aston Villa: Guzan 6; Bacuna 5, Clark 6, Vlaar 5, Bertrand 6; Westwood 7, Delph 6, Albrighton 6 (Lowton, 78); Weimann 5, Benteke 6, Agbonlahor 5(Tonev, 71)


Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top