Picha za ajali mbaya ya gari nchini brazil

Ajali ya kutisha imetokea huko nchini Brazil leo majira ya saa 10:00am kwa saa za Afrika mashariki baada ya gari aina ya Toyota Hilux Pickup kupinduka katika barabara kuu ya state highway 010.

Kwa mujibu wa dereva wa gari hilo ambae aliomba jina lake lihifadhiwe  alisema,ndani ya gari hilo kulikuwa na watu sita,yeye mmoja na wengine watano.

Dereva huyo aliendelea kunyetisha kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi,ambapo alishindwa kulidhibiti gari hilo lilipodumbukia katika shimo kubwa lililokuwa katika barabara hiyo na kupinduka.
Majeruhi wote waliokolewa na kikosi cha zimamoto nchini humo na kupelekwa katika hospitali ya HPS Ana granddaughter iliyopo Bueno nchini Brazil.

Alipohojiwa na polisi alisema kuwa gari lilikuwa jipya na halikuwa na muda mrefu tangu liliponunuliwa kutoka dukani hivyo hakuwa na bima (insurance).

Baadhi ya watu walioshuhudia ajali hiyo walimlaumu dereva huyo kwa kutembea mwendo kasi lakini pia waliilaumu serikali kwa kutoziba mashimo mengi katika barabara hiyo kuu kwani hicho ndio chanzo kikubwa cha ajali nchini humo.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top