Wema Sepetu amwaribia siku Pastor Muyamba...... soma zaidi hapa

 Wema Sepetu
STAA wa filamu nchini, Wema Sepetu hivi karibuni alimuharibia siku Emanuel Myamba maarufu kama Pastor Muyamba, kwa kushindwa kufika kwenye hafla iliyokuwa imeandaliwa na chuo chake cha sanaa ‘TFTC’ akiwa kama mgeni rasmi.

Mtoa habari amesema  kuwa, Wema aliombwa na kukubali kuhudhuria shughuli hiyo, lakini alipopigiwa simu dakika za mwisho aliwaambia kwamba atashindwa kufika kwa kuwa amefiwa na shangazi yake udhuru ambao baadaye ilibainika kuwa haiukuwa ya kweli.

Amesema kutokana na kutofika kwa staa huyo, ambaye hata hivyo mwaliko wake ulitokana na shinikizo la wanafunzi wa chuo hicho, walilazimika kuwaomba radhi wageni wengine, wakiwemo waandishi wa habari.

Mmoja wa watu wa karibu na Wema alisema kuwa muigizaji huyo hajawahi kupatwa na msiba siku za hivi karibuni, kwani mara zote amekuwa akiwaeleza kila linapotokea jambo zito kama hilo.
 
                                              Emanuel Myamba
Mtu huyo amesema katika ratiba ya siku hiyo, walikuwa waende kwenye tukio moja la starehe na halikuwa limebadilika. juzi alipoulizwa Pastor Myamba alikiri Wema kutofika kwenye hafla hiyo kitendo alichosema kimemsikitisha kwani walitoa mwaliko kwake kutokana na heshima aliyonayo.

“Nimemshangaa sana, lakini mbona mwenzake Jokate alikuja, ni kwa sababu anajitambua na ni professional,” amesema Myamba.



TUNAOMBA MAONI YAKO HAPA CHINI KUHUSU TAARIFA HII!!! 

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top