HATARI: Kijana auawa akituhumiwa kwa Imani za kishirikina‏

Matukio ya kujichukulia sheria mikononi bado yanazidi kuyakumba baadhi ya maeneo mkoani Mbeya ambapo katika tukio la jana  kijana  wa miaka 39 ameuawa na wananchi wenye hasira kali wakimtuhumu kwa imani za kishirikina.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi, amethibitisha kutokea kwa kifo hicho na kumtaja marehemu liyetambulika kwa jina la Gabriel Mwandemwa (Mwasyebule) mkazi wa kijiji cha Ikamambande Wilaya ya Rungwe aliuawa na watu wasiofahamika kwa kukatwa na vitu vyenye ncha kali sehemu za kichwani na kifuani.
Marehemu Gabriel Mwandemwa(Mwasyebule) enzi za uhai wake, Marehemu alikuwa akijishughulisha na biashara mbali mbali ikiwemo uuzaji wa maziwa na ununuzi wa mahindi.

Alisema tukio hilo lilitokea jana majira ya saa tano asubuhi huko katika Kijiji cha Ikamambande, kata ya Lwangwa, Tarafa ya Busokelo, Wilaya ya Rungwe, mkoani hapa.
Alisema taarifa za awali zinadaiwa kuwa, uongozi wa kimila kijijini hapo  uliitisha kikao cha dharura ukihusisha viongozi wa vitongoji na vijiji jirani na ndipo waliamua kumtafuta na kumlazimisha marehemu kuhudhuria katika kikao hicho na kisha kuanza kumpiga na kupelekea kifo chake.
Alisema marehemu alikuwa akituhumiwa kuwa ni mshirikina kijijini hapo kwa kuwa anawaroga watoto na kuwa anajipatia mazao mengi kwa kuwatumikisha watu kishirikina.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top