Man united imekubali kipigo cha 5-3 dhidi ya Leicester City

Ligi kuu ya Uingereza imeendelea tena jioni ya leo kwa mchezo kati ya Manchester United dhidi ya timu iliyopanda daraja ya Leicester City.Ambapo leo hii Man U wamepokea kipigo kizito kutoka kwa Leicester, baada ya kukubali kufungwa 5-3.
Man U ndio waliokuwa wa kwanza kuliona lango la Leicester kupitia Robin van Persie,Angel di Maria kuongeza la pili.

Dakika moja baada ya United kufunga goli la pili, Leicester wakafungw goli la kwanza kupitia Ulloa na mpaka mapumziko matokeo yalikuwa 2-1.

Kipindi cha pili Ander Hererra akaifungia Man United goli la 3, lakini dakika chache baadae Leicester wakapata penati na kufunga goli la pili, huku United wakiwa bado na hasira za kulalamikia maamuzi ya refa, Estaban Cambiasso akafunga goli la kusawazisha.

Mchezaji aliyeng’ara kwenye mchezo Jamie Vard akaifungia City goli la 4, Nugent kufunga goli la tano kwa mkwaju wa penati.

Mpaka mpira unaisha dk 90 Leicester City 5-3 Man United.

Leicester: Schmeichel 6, De Laet 6.5, Morgan 6, Moore 6, Konchesky 6, Hammond 6.5, Drinkwater 7.5, Cambiasso 7.5 (King 6), Nugent 7.5 (James 6) , Ulloa 7.5, Vardy 8.5 (Schlupp 6).

Man U: De Gea 5.5, Da Silva 4.5, Evans 5 (Smalling 5), Blackett 4.5, Rojo 4, Blind 6, Ander Herrera 7, Di Maria 8 (Mata 5), Rooney 7, Falcao 7 (Januzaj 5), Van Persie 7.5.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top